Sunday, May 1, 2016

MATATIZO YA KISAIKOLOJIA
Na fredy salvatory
makala na chanzo cha  gazeti
Kukubali na Kukabili matatizo ya Kisaikolojia
     
  Matatizo ya kisaikolojia ni nini?
   Matatizo ya kisaikolojia ni yale yanayoathiri ufahamu wa mtu na uwezo wake wa kufikiri,kupambanua mambo au kufanya uamuzi katika shughuli zake za kila siku.Matatizo ya kisaikolojia huweza kutokea katika hatua yoyote ya maisha ya binadamu kuanzia utoto hadi uzee.Matatizo ya kisaikolojiaa huweza kusababishwa na mambo mengi.Baadhi ya mambo hayo ni
1.     Ukosefu wa chakula bora.Chakula bora huwa na virutubisho,kama vile madini na vitamini ambavyo huimarisha afya ya ubongo na kutafanya tuwe na hali ya utulivu kiakili
2.     Ubongo kukosa damu ya kutosha ambayo husambaza virutubisho,oksijeni,na kuondoa kabonidayoksaidi,hivyo kuufanya kushindwa kufanya kazi ipasavyo
3.     Majeraha kichwani yanayotokana na ajali
4.     Kupotea mtu unayempenda au unayemtegemea,kwa mfano kufiwa na mzazi/wazazi,walezi  au ndugu wa karibu
5.     Tukio la kuumiza au kusikitisha kwa mfano kufeli mtihani,kubakwa,kuibiwa mali,kuteswa au kugundua kuwa una ugonjwa usionatiba
6.     Kuvunjika kwa ndoa hivyo watoto kukosa msimamo na mashauri au msimamizi
7.     Ugomvi kati ya wazazi
8.     Kutelekezwa
9.     Mazingira yasiyo salama kwa mfano vita na majanga ya asili kama vile mafuriko,kimbunga na milipuko ya volcano.
10.         Utumiaji wa dawa za kulevya.                                            Matatizo ya kisaikolojia huweza kuleta madhara mengi,yakiwemo kupata ulemavu,shinikizo la damu,maumivu  ya mwili,kushindwa kusoma au kufanya kazi,kukosa marafiki,kukosa furaha na amani au hata kupoteza maisha.
Dalili za mtu mwenye matatizo ya kisaikolojia.   
·       Kuwa na hasira inayopindukia
·       Kuhamaki kwa mambo madogo na hata ya kawaida
·       Kuwa na huzuni na kujiona huna thamani kwa jamii
·       Kuchanganyikiwa na kukosa usikivu au umakini
·       Kujitenga na wengine na kushidwa kujenga uhusiano,kwa mfano kuwa na marafiki
·       Kuwa na wasiwasi na uoga uliopindukia mara kwa mara
·       Kukosa usingizi na kuweweseka wakati ukiupata
Aina za matatizo ya kisaikolojia.
         Kuna aina mbalimbali za matatizo ya kisaikolojia.Baadhi ya aina hizo ni wasiswasi,mafadhaiko na utukutu
MATATIZO YA KUWA NA WASIWASI
Wasiwasi ni jambo la kawaida kwa mwanadamu.Hata hivyo kuna wakati mtu huwa na wasiwasi na hofu kuliko kawaida hata kwa vitu ambavyo ni vya kawaida hata kwa vitu ambavyo na vya kawaida sana au vitu ambavyo havipo kabisa.Inapofikia hali hiyo,tunaweza sema mhusika ana ugonjwa wa wasiwasi.
Dalili za ugonjwa wa wasiwasi
1.     Kuogopa vitu vya kawaida kama vile wanyama ,(mbwa,nyoka,au mende),kupanda majengo marefu,au kuogopa kukaa kwenye chumba cha pekee yako au kwenye lifti
2.     Aibu isiyo kuwa ya kawaida
3.     Kushindwa kutulia
4.     Kukosa usingizi
5.     Kuhisi kizunguzungu na kutokwa jasho

 UGONJWA WA MAFADHAIKO
Mfadhaiko ni tatizola kisaikolojia linalotokana na msongo wa mawazo kutokana  na tukio la kuhuzunisha,kama vile kufiwa,kufeli mitihani,kukataliwa,kutelekezwa na mme/mke.Kwa kawaida watu hupatwa na huzuni kutokana na matukio ya kusikitisha na hurejea katika hali yao ya kawaida baada ya muda.Hata hivyo watu wenye mafadhaiko hushindwa kukubali hali yao ya kawaida baada ya muda.



               Dalili za mtu mwenye mafadhaiko
·       Uchovu
·       Kuhisi upweke na kujiona huna thamani hata kutamani au kujaribu kabisa kujiua
·       Kutotamani kufanya kitu chochote, hata kazi au mambo ambayo ulikua unayapenda.Watoto huwa hawapendi kucheza au kufanya kazi za shule
·       Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.Baadhi ya watu huweza kula sna kuliko kawaida
·       Kushidwa kufukiri, kutokua  kuwa makini na kufanya uamuzinjuu ya mambo ya maisha yake ya kila siku
·       Kushindwa kupata usingizi lakini  baadhi hulala kuliko kawaida
·       Kujiona kuwa  ni mbaya na huwezi kufanya kiyu chochote kizuri chenye manufaa


 TATIZO LA UTUKUTU                                      
Kwa kawaida watoto ni watundu.Utukutu ni utundu usio wa kawaida ambao muda wote mtoto hushidwa kutulia na hata kufanya vitendo vya hatari au uharibifu.Baadhi ya wtoto wenye tatizo hili la utukutu,hulazimika kupelekwa hata jela ya watoto ambako hupewa mafunzo maalumu ili waweze kuishi maisha ya kawaida.Kukubali na kukabili matatizo ya kisaikolojia ni muhimu kudhibitiwa,huathiri afya zetu,mihemko,uhusiano  na wengine,uzalishaji mali,maisha kwa ujumla na hata kusababisha matatizo kwenye familia.Matatizo ya kisaikolojia yanaweza kudhibitiwa na mtu kuendelea na maisha yake kama kawaida.Matatizo kutafita n ya kisaikolojia  kudhibitiwa na mtu kuendelea na maisha yake kama kawaida.Matatizo hayo ni kukubali tatizo na kuwa tayari kukubaliana nalo.Zifuatazo ni baadhi ya njia za kukubaliana na matatizo ya kisaikolojia
·       Kukubaliana na hali halisi ingawa umepata tatizo inabidi kutafuta njia sahihi ya kuondoa na kulisahau tatizo hio
·       Epuka kujitenga bali shirikiana na kuchanganyika na watu.Hii husaidia kupunguza huzuni au mihemko
·       Omba msaada au ushauri kutoka kwa watu wa karibu au unaowaamini,kwa  mfanorafiki,ndugu,mshauri nasaha au kiongozi wa dini.Waeleze jinsi unavojisikia na fanyia kazi mashauri yao
·       Jiwekee ratiba ya kila siku na uitekeleze,usipote mda kwa kukaa bure
·       Fanya mazoezi,pata usingizi wa kutosha na muda wa kupumzika pamoja na muda wa kusirikiana na watu katika shughuli za kijamii
·       Imarisha afya yako kwa kula chakula bora,epuka ulevi na dawa za kulevya kwani huongeza ukubwa wa tatizo

·       Waone wanasaikolojia

Thursday, April 28, 2016


NA JENESTA ZEDEKIA.
Halmashauri nchini katika ngazi ya wilaya na vijiji na  kata wametakiwa   kuona  umuhimu na kutoa kipaumbele  katika sekta  ya mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutoa elimu kwa jamii ili kupinguza uharibifu wa mazingira .



Baadhi ya wahitimu walio pata mafunzo katika semina hiyo
Hayo yamesemwa na mkurugenzi shirika  linatoa  hudumu  mabadiliko ya tabia ya nchi utawala bora uchumi kwa wanawake na vijana SOTAS  Jackison Muro wakati  akizungumza katika semina iliyofanyika katika halmashauri ya wilaya ya meru mkoani arusha

Zakaria fausitine meneja wa program ya ufugaji asili
 Mkurugenzi   muro amesema lengo la semina hiyo kujadiliana jinsi ya sekta ya mabadiliko ya tabia nchi itakapoingizwa katika mpango wa halmashauri na bajeti za halmashauri katika ngazi ya vijiji na wilaya.
Awali akifungua semina hiyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bakari Salim  amewataka wananchi kuachana na biashara za  kukata miti pamoja na kuchoma mikaa kwani hiyo yote ni uharibifu wa mazingira.

Baadhi ya madiwani walioodhuria katika Semina hiyo akiwemo diwani wa kata ya Makiba Emannuel Pendael Molel  wamesema kuwa wataenda kuwa chachu katika kata zao kwa kutoa  elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira.

Tuesday, April 26, 2016

Serikali yatakiwa kuweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali.

Na fredy salvatory

Serikali imetakiwa kuweka mazingira rafiki kwa wananchi wote wanaojishugulisha  na biashara ndogo ndogo maarufu kama ujasirimali ili kuwafanya kuwa na wigo mpana  wa kuweza kukubaliana na hali ya maisha pamoja na kuchagia katika shughuli za kimaendeleo.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na baadhi ya wanawake ambao wanajishugulisha na biashara ndogondogo ya kulima nakuuza mbonga  za majani  maarufu kama wajasiriamali jijini Arusha katika mahojiano na blog hii.

 Walisema  licha ya kujenga mazingira mazuri ya kufanya biashara  lakini wanatakiwa kuangaliwa kwa upande wa mikopo itawezesha kupanua na kukuza biashara yako na kujikimu kimaisha na kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi ‘Tunaiomba serikali kuhakikisha  inatuwekea mazingira  kwa watu tunao jishughulisha hizi ndogondogo pamoja nashughuli zote za  ujasiliamali kwani inatusaidia  kuondokana na wimbi la umasikini  pia tutakuwa na wasaa wakuchangia michango katika shughuli za kimaendeleo’ alise moja ya  mwana mama mjasiriamali  aliejitambulisha kwa jina la Mama Rehema.

Alisema wakiwekewa mazingira mazuri na rafiki katika serikali wataweza kujiajiri wenyewe na  kuondoa dhana  ya kusubili kuajiriwa na mtu au kuajiriwa na serikali huku wakiwataka wanawake wote kuwaiga wao kwa  kujishughulisha na shughuli mbalimbali ili kuziendeleza familia zao na kutokuwa tegemezi alisema mama huyo na kuongeza kuwa kwasasa imepita miaka kumi (10) toka aanze kufanya biashara hiyo huku akidai kupitia biashara yake hiyo anasomesha watoto wake wawili mmoja akiwa  katika  shule ya sekondari na mwingine akiwa katika shule ya  msingi.


Aidha mama huyo alisema kuwa kipindi hiki  serikali iweze kuwawekea hata maeneo ya kufanyia biashara  pasipo kukimbizwa na kuwakosesha amani wawapo katika biashara na kuwaasa wanawake kujitambua na kuwataka kuungana kuwa na vikundi vitakavyo  wasaidia kukuza miladi yao na kuwa namichango kwaajili ya kuendeleza miladi yao.Nakusema kuwa mkiwa na vikundi wanawake mnakuwa sitegemezi katika familia  naendapo mtu akitaka kufanya mladi huunmganisha mawazo na kujiendereza kimaisha na katika kuinua uchumi wa familia na nchi jumla. 

Friday, April 22, 2016

IFAHAMU ASALI KAMA TIBA NA SIYO ZAO. 


Makala haya yameandaliwa na John Billah 

Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza ukajiuliza maswali mengi ya msingi ni kwa nini nimeamua kuandika makala yenye kichwa cha habari kama hiki kwa siku a leo,lakini jibu la msingi yamkini waweza kuwa ni mmojawapo ya watu wanaoichukulia asali kama ni sehemu ya kiburudisho katika matumizi yao ya kila siku ,ikiwa ni pamoja na kuilamba ,kuitumia kwenye uji kama sukari mbadala kwa kinywaji.

La hasha ndugu mpenzi msomaji wa makala hii napenda kukukaribisha katika safu hii ya makala mahsusi iliyojikita katika Suala zima la zao la asali pamoja na faida zake katika maisha ya mwanadamu yenye kila aina ya nakshi hapa duniani .

Asali ni zao mojawapo linalotengenezwa na mdudu fundi anayejulikana kwa jina la Nyuki kwa kutumia vitu kadha wa kadha kama vile maua ,mbegu za miti,ua za matunda mbalimbali,mbarawa ikiwemo vitu vyenye asili ya chumvi pamoja na vitu vyenye asili ya majimaji ili kuunda asali ambayo leo hii mimi na wewe tunaitumia kwa matumizi .

Na pia asali hii imeweza kugawanywa katika makundi makuu mawili na wataalamu mbalimbali wahusuyo mambo ya nyuki na asali,mbayo kundi la kwanza ni asali inayo tengenezwa na vyanzo vya nyuki wenyewe kutoka porini aidha kuiandaa katika mapango ,magome ya miti,pamoja na mizinga ya kuchongwa na mwanadamu ambayo huianika kwa taraji la nyuki kupata hifadhi kwa ajili ya kutengeneza asali katika sehemu hizo husika.


Pia kundi la pili ambalo wataalam wamefafanua ni ile asali ambayo hupatikana kwa njia ya kuandaa masanduku mahsusi ,maboksi pamoja na mizinga y kuchongwa na watu binafsi,makampuni ,taasis ,na mashirika au miradi ya ufugaji nyuki na kwenda kuianika sehemu ambazo ni shawishi kwa ajili ya makazi ya wadudu nyuki ili waweze kutengeneza asali ambayo kwa kitaalam tunaita ni asali ya nyuki ya kufugwa kutokana na elimu  ya ufugaji nyuki.

Mbali ya mimi na wewe kuitumia asali kama sehemu ya kiburudisho ,ukweli ni kwamba asali ni zao pekee duniani kama chakula chenye kukaa muda mrefu pasipo kuharibika au kuoza kwa haraka pasipo kujali ni wapi zao hili limehifadhiwa kwa matumizi ya kila siku.

Asali licha ya kuwa ni rafiki wa karibu kwa maisha ya mwanadam ,tambua asali ni mojawapo ya tiba murua kwa huduma ya awali kwa mhanga wa ajali yeyote wa majeraha ya moto,hutumika kumpaka ili kupunguza maumivu makali katika jeraha la mtu aliyeungua moto maana huvuta maumivu makali ya moto kwa asilimia 55 hadi asilimia 90.kabla ya kumuona daktari kwa ajili ya tiba kwa kina.

Pia asali hutumika kama dawa ya kikohozi kwa mtu yeyote anayepitia adha ya ukavu wa kikohozi kigumu wakati wa kukohoa ,maana asali huchanganywa na yai bichi na ndipo mgonjwa akipatiwa inakuwa ni tiba tosha kwa kuuondoa kikohozi kigumu au kwa mtu ambaye sauti yake ipo chini sana kwa ajili ya kukohoa muda mrefu.


Kwa tamaduni ya jamii ya watu waishio maeneo ya vijijini hupenda kuitumia asali kama sehemu kuu ya matumizi kwa ajili ya kuandaaa kifungua kinywa ikiwa ni pamoja na kuitumia katika uji kama sukari mbadala,kuipaka kwenye mikate ,na kubwa zaidi huitumia asali katika matumizi ya kinywaji aina ya pombe ya kienyeji ili kuongeza makali ya pombe iweze kuwa na kilevi kikali zaidi.

Na sanjari na hapo mwanadamu anashauriwa kila siku iendayo kwa Mungu awe anapata angalau kijiko kimoja cha asali ili kuweza kmpungumzia maradhi mbali mbali yaliyopo ndani ya mwili wake ikiwa ni pamoja na kusafiha mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuratibu kiwango cha sukari mwilini.

Naam mpenzi msomaji wa safuu hii ya makala kuhusu zao la asali kwa leo tukomee hapa ,chukua hatua thubutu kwa kuitumia asali kila siku na uwe nayo ndani ya nyumba yako kama rafiki wa afya wa karibu ,maana siku zote mchawi wa maisha yako ni wewe binafsi……,tukutane wakati ujao upate kujua zao hili linapatikana wapi hapa Tanzania?????.

Friday, April 15, 2016

chanzo na bbc,swahili


Aliyemkejeli Rais Erdogan kushtakiwa
  • 15 Aprili 2016
Image copyrightReuters
Image captionMchekeshaji Jan Boehmermann.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel anasema kuwa serikali ya ujeremani imeidhinisha kufanyika uchunguzi dhidi ya mchekeshaji aliyemfanyia kejeli rais wa Uturuki .
Kisheria serikali ni lazima iidhinishe matumizi ya kipengee chochote cha sheria wakati wa kukejeliwa kwa kiongozi wa nchi nyingine.
Bi Merkel, amasema kuwa mahakama ndizo zina uamuzi wa mwisho. Uturuki ilitaka kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya rais Recep Tayyip Erdogan kukejeliwa.
Image copyright
Image captionRais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Waendesha mashtaka wataamua ikiwa wataendelea na kesi dhidi ya mchekeshaji huyo Jan Boehmermann, ambaye alitumia shairi kumkejeli rais Erdogan.
Ikiwa atapatikana na hatia, atapigwa faini au kufungwa jela. Baadhi ta wataalamu wanasema kuwa ana uwezo wa kujitetea kwa kuwa, shairi hilo linaonekana kuwa kichekesho kuhusu uhuru wa kusema na wala sio kejeli.

Tuesday, April 12, 2016

Ombaomba kuondoka jijini dar ifikapo jumatatu

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameamuru watu wanaoomba mitaani katika maeneo mbalimbali jijini wakamatwe, waache kufanya shughuli hiyo isiyo halali. Ameagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kuanzia Jumatatu, waanze kuwakamata ‘ombaomba’ hao .
Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam, alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema watu hao wanaosimama barabarani katika maeneo ya jiji, muda wao umefika kikomo kwani maeneo hayo si sahihi kwa ajili ya shughuli hiyo.
Alisema ni vyema watu hao wakaenda katika vituo mbalimbali vilivyoanzishwa na wasamaria kwa ajili ya wenye uhitaji badala ya kusimama mitaani katika maeneo ya jiji kuomba. “Nimegundua kuwa asilimia 80 ya ombaomba wamekuja Dar es Salaam na nauli zao hivyo naomba warudi kwa nauli zao na hao asilimia 20 waende kwenye hivi vituo,” alisema Makonda.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwataka ombaomba hao kuondoka wenyewe bila kusubiri kuondolewa na Polisi. Pia aliwataka wenyeviti wa Serikali za mitaa kuanza wenyewe kuwaondoa kwa kusema kwani kuendelea kuwaacha kunasababisha kujaa na kuleta kero.
“Msisubiri Polisi wafanye kazi hiyo pekee yao, lazima na wenyeviti mshiriki kuwaondoa na ninaamini tukishirikiana tutawaondoa wote na jiji litabaki shwari,” alisema Sirro. Agizo hilo la kuwakamata wanaoomba mitaani, limekuja baada ya hivi karibuni Makonda kupiga marufuku wapitia njia kuwapatia fedha watu hao, ambao wengi wamekuwa wakitumia watoto wadogo kuomba.
Agizo la kutaka omba omba wakamatwe kuondokana na vitendo hivyo jijini, limewahi kutolewa pia na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba ambaye aliamuru waondolewe warudishwe wanakotoka.
Hata hivyo jiji hilo la Dar es Salaam limeendelea kugubikwa na wimbi la watu hao wanaoomba ambao baadhi wamekuwa wakitumia watoto wadogo ambao huvizia watu na kuwaomba fedha.
Bomoa bomoa Katika hatua nyingine, Makonda amewataka watu wote waliojenga magorofa bila maeneo ya maegesho ya magari, kufika katika ofisi yake Jumatatu kujadili kubomoa majengo yao au kulipa faini na kujenga maegesho hayo.

Sunday, April 3, 2016

LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA  MKOA ARUSHA HATIMAE IMEFIKA KI LELENI


03/04/2016

 Michuano iliyokuwa ikiendelea jijini Arusha ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa ambapo jioni ya leo imezikutanisha timu nne, mbili zikiwa zimegongana pointi, timu hizo zilizo kipiga  katika viwanja viwili tofauti moja ikichezea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid na mchezo mwingine ukichezwa kwenye uwanja wa Iliboru.

Katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid umezikutanisha timu ya Karatu United   na timu ya Nyota Fc,Mtanange huo ulikuwa wavuta nikuvute kila timu ikitaka kuibuka na ushindi ambapo timu ya Karatu ilipo wazidi ujanja wapinzani wao na kujipatia goli moja 1-0  kupitia kiungo  mshambuliaji John Thomas John ambaye amewapatia goli hilo lilodumu hadi dakika  90 za mchezo huo.

Kocha wa timu ya Karatu  amesema walichokuwa wanakitaka ni kuweka heshima ya Karatu united mchezo huo ulikuwa muhimu kwao kuliko michezo mingine nakuwaomba wadau wa karatu united  kujitokeza kusaidia timu hiyo ili katika msimu ujao iweze kufanya vizuri katika mashindano ya ligi ngazi ya mkoa

Vilevile amewaasa viongozi wa mpira kuwa waungwana hasa waamuzi wawapo uwanjani kwani timu zinatumia gharama nyingi kwa ajili ya mashindano na pindi wanapo panga matokeo inakatisha tama timu shiriki.

PICHA WACHEZAJI WA KARATU UTD


Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Ilbolu ambao uilikuwa unafuatiwa na washabiki wengi ulikuwa kati ya klabu ya Pepsi na klabu ya Chakyi fc uleweza kumalizika kwa klabu ya Pepsi fc kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kufanikiwa kutoa ubingwa wa mkoa wa Arusha baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 16 katika ligi hiyo 

Friday, April 1, 2016

Balozi Seif ahimiza uadilifu kufanikisha malengo


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka watendaji wa taasisi za umma nchini kuwa makini zaidi katika kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha kwenye taasisi.
Alitahadharisha kwamba kipindi hiki hali ya fedha si nzuri kutokana na mambo mengi yaliyofanywa katika kipindi kifupi kilichopita ikiwemo suala la uchaguzi mkuu ambalo limelazimika kutumia fedha nyingi, zaidi baada ya kujitokeza wa uchaguzi wa marudio.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa watendaji wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake walipompokea rasmi kuingia ofisini kwake na kuanza kazi mara baada ya kuteuliwa tena na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein kushika wadhifa huo katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuendesha taasisi zake za Umma kwa kutumia fedha inazokusanya kupitia vianzio vyake mbalimbali chini ya usimamizi wa watendaji watakaoonesha uadilifu kwenye usimamizi huo.
Ametaka taasisi za fedha ikiwemo bodi ya mapato na mamlaka ya kodi nchini TRA kuwa wabunifu zaidi katika kutafuta fedha katika vyanzo vipya kwa lengo la kuona Serikali inatekeleza malengo yake vizuri ili kupambana na baadhi ya washiriki wa maendeleo ambao wametishia kusitisha misaada yao kwa kisingizio cha uchaguzi wa marudio.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kuchukiwa kwake na baadhi ya watendaji wa Umma wenye tabia mbaya ya kuwekeana chuki katika utekelezaji wa majukumu yao yanayowakabili ya kila siku, hatua ambayo husababisha kushuka kwa utendaji na uzalishaji sehemu za kazi.
Balozi Seif pia aliwapongeza na kuwashukuru viongozi pamoja na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake kwa kazi kubwa waliyoifanya iliyomuwezesha kutekeleza majukumu yake ya ufanisi mkubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.
Mapema Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Ahmad Kassim kwa niaba ya watendaji wa ofisi hiyo amempongeza Balozi Seif kwa kuteuliwa tena kushika wadhifa huo hatua ambayo inaonesha uwezo wake katika kusimamia shughuli za serikali.

Thursday, March 31, 2016

CHACKYI YA JIJINI ARUSHA YAZIDI KUWANG’ALISHA MASHABIKI WAKE LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA KATIKA UWANJA  WA SHEIKH AMRI ABEID
Arusha.
30.03.2016.

Na Fredy salvatory.

Michuano ya ligi daranja la tatu ngazi ya mkoa wa Arusha kumtafuta bingwa wa mkoa kwa ajili ya kushiriki ligi daraja la pili Tanzania bara imeendelea kutimua vumbi ambapo hapo jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini  Arusha .
Katika mchezo uliochezwa jana ulizikutanisha klabu ya Charky inashika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 10 kibindoni dhidi ya klabu ya Monacti fc wanaoshika nafasi ya nne  wakiwa tayari wameshajikusanyia  pointi nne .
Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute kutokana na kila timu kuhitaji kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutoa ubingwa ulimalizika kwa klabu ya Chakyi kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya wapinzani wao klabu ya Monacti ambao hawakuambulia chochote katika mchezo huo.  


wakienda mapumziko kipindi cha kwanza chackyi wakiongza magori mawili  2-ya kipindi hicho cha kwanza cha mchezo


Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Chakyi Rashidi Chama  alizungumzia mchezo huo na kusema  timu yake imejipanga vizuri na anamatumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa siku ya jumamosi na pia alisema tatizo la timu nyingi kujitoa katika mashindano inasababishwa na kuwa na viongozi ambao sio wanamichezo.
Kwa  upande wake katibu wa mashindano hayo kwa mkoa wa Arusha  Maki Warioba alisema kuwa timu ambazo zilikuwa zinashiriki katika mashindano hayo ni nane na baadae timu moja kujiondoa katika ligi hiyo baada ya kushindwa kucheza mchezo mmoja ambayo ni Arusha Meet  mpaka sasa zimebakia  timu saba.
Matokeo hayo yalionekana kuinufaisha club ya Chackyi ambayo iliweza kufikisha point 10 nyuma ya vinara wa ligi hiyo ambao ni club ya pepsi ambao tayari walijikusanyia point 13 katika ligi  daraja la tatu ngazi ya mkoa.


Sunday, March 27, 2016

Yanga yaitega Al Ahly


KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ameandaa mbinu tatu kuiangamiza Al Ahly ya Misri kwa ushindi wa kishindo zitakapokutana katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo huo utafanyika Aprili 9, mwaka huu, Uwanja wa Taifa uliopo Wilaya ya Temeke Dar es Salaam, kisha zitarudiana wiki mbili baadaye mjini Cairo, Misri.
Akizungumza na gazeti hili, Pluijm alisema sababu ya kuandaa mikakati hiyo ni kutokana na ubora na uzoefu waliokuwa nao Al Ahly ambao kwa sasa wanafundishwa na Mholanzi mwenzake Martin Jol, aliyewahi kuzifundisha timu za Tottenham na Fulham zinazoshiriki Ligi Kuu ya England.
“Huu ni mchezo mkubwa na tunakutana na timu yenye rekodi nzuri Afrika na wachezaji na kocha mwenye uzoefu mkubwa, hivyo ni vyema tukajipanga kwa kuwa na mbinu nyingi za kivita,” alisema.
Alisema anachotaka ni kuona timu yake inapata ushindi wa mabao yasiyopungua matatu nyumbani ili waweze kuwa na kazi nyepesi ya kulinda ushindi wao mchezo wa marudiano.
Alisema katika kuhakikisha mipango yake inafanikiwa anachokifanya kwa sasa ni kuliandaa jeshi lake hasa kikosi kitakachoanza siku hiyo ili kicheze na kutimiza majukumu atakayowaelekeza. “Nawajua Al Ahly, ni mara ya pili sasa tunaenda kucheza nao siyo timu mbaya, lakini hawatishi kama inavyozungumzwa mitaani.
“Najua mbinu za kocha wao wa sasa ni rafiki yangu, Mholanzi mwenzangu ingawa yeye hazijui za kwangu kwa hiyo naamini tuna nafasi nzuri ya kuweka rekodi ya kuwatoa na kucheza hatua ya makundi mwaka huu,” alisema Pluijm.

Wednesday, March 23, 2016

Waziri Nape awaahidi neema muziki wa dansi



WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kupambana na kila aina ya udhalimu unaoikabili tasnia ya muziki wa dansi nchini.
Nape alitoa ahadi hiyo katika mkutano wake na wanamuziki wa dansi uliofanyika juzi katika ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni, Dar es Salaam.
Alisema kutokana na mchango mkubwa wa muziki wa dansi katika nchi hii unastahili heshima na wanamuziki wake kuwa na maendeleo makubwa.
Aliongeza kuwa tofauti na inavyotarajiwa, muziki huo umekuwa ni kama wa kawaida huku wasanii wake kila kukicha wakiwa na malalamiko ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka.
Nape alisema hayo baada ya kupokea malalamiko kadhaa kutoka kwa wanamuziki wa muziki huo.
Akiendelea kujibu kero kadhaa, alisema kuwa kodi, uharamia, kudhulumiwa pamoja na kutopewa kipaumbele katika vituo vya redio ni moja ya changamoto kubwa za muziki huo.
Akizungumzia kuhusu kodi, alisema kwa kuwa serikali inahitaji mapato kutoka katika kila sekta, hawezi kuwasaidia kuondoa kodi ya kuingiza vyombo vya muziki ila anaweza kusaidia kupatikana urahisi wake. Pia akizungumzia kutopewa kipaumbele kwa nyimbo za dansi katika redio, aliwataka wasanii hao kumuachia suala hilo.
Pia aliongeza kuwa: “Nimeamua kuja kuwasikiliza mwenyewe kama Waziri wenu na ninataka kuwahakikishia kuwa harakati za Rais John Magufuli za kuwasaidia zitafanikiwa tu, na kazi ndio inaanza,” alisema.

Monday, March 21, 2016

Rais Magufuli atii agizo la Makonda



RAIS John Magufuli amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuhakiki silaha baada ya bunduki zake mbili aina ya Shot gun na bastola kuhakikiwa nyumbani kwake Ikulu, Dar es Salaam.
Uhakiki huo umefanywa na maofisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro. Akizungumza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, Rais Magufuli alimpongeza Makonda na Jeshi la Polisi kwa kuendesha uhakiki wa silaha, na alitoa mwito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchi nzima kuhakikisha zinahakikiwa.
Makonda juzi alitoa miezi mitatu kwa wenye silaha kuhakiki silaha zao na muda huo utamalizika Julai Mosi mwaka huu. Rais Magufuli pia alilitaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
“Ni aibu kumuona askari Polisi mwenye silaha ananyang’anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang’anye silaha na wewe una silaha?” Amehoji Rais Magufuli.
Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Sirro alimshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono kazi hiyo na alisema Polisi imejipanga kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa mafanikio.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametaka pande zinazogombea kiti cha Umeya katika Jiji la Dar es Salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika leo badala ya kuendelea kulumbana.
Dk Magufuli alisema upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo ili Meya apatikane na Jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.
“Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli,” aliongeza Rais Magufuli.
Wakati huo huo, Mwandishi Wetu, Flora Mwakasala anaripoti kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la kuzuia uchaguzi wa umeya na unaibu meya wa Jiji la Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika leo, na kuamuru uchaguzi huo ufanyike kama ulivyopangwa.
Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, kwa kuwa Mahakama imeona hakuna sababu zozote za msingi zilizowasilishwa na walalamikaji kuzuia uchaguzi huo.
Maombi ya kuzuia uchaguzi huo yaliwasilishwa jana mchana na Suzan Massawe na Kumjhi Mohammed kupitia kwa Wakili wao Elias Nawela dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
Katika maombi yao, waliiomba Mahakama itoe zuio la kufanyika uchaguzi huo pia iamuru hali ibaki kama ilivyo hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi, kwa kuwa walalamikaji katika kesi hiyo, hawajapewa haki yao ya kualikwa kushiriki katika uchaguzi huo.
Akisoma uamuzi huo, Hakimu Lema alisema Mahakama haioni sababu za msingi zilizowasilishwa na walalamikaji kuzuia kufanyika kwa uchaguzi huo pia hawajaleta uthibitisho kama wao siyo miongoni mwa wapiga kura.
Aidha alisema, kulikuwa na kasoro nyingi ikiwemo kukosekana kwa orodha inayoonesha majina ya wapiga kura, jambo lililosababisha Mahakama kutokujua kama waleta maombi ni miongoni mwa wapiga kura.