NA JENESTA ZEDEKIA.
Halmashauri nchini katika ngazi ya wilaya na vijiji na kata wametakiwa kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika sekta
ya mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutoa elimu kwa jamii ili kupinguza
uharibifu wa mazingira .
Baadhi ya wahitimu walio pata mafunzo katika semina hiyo
Hayo yamesemwa na mkurugenzi shirika linatoa
hudumu mabadiliko ya tabia ya
nchi utawala bora uchumi kwa wanawake na vijana SOTAS Jackison Muro wakati akizungumza katika semina iliyofanyika katika
halmashauri ya wilaya ya meru mkoani arusha
Zakaria fausitine meneja wa program ya ufugaji asili
Mkurugenzi muro
amesema lengo la semina hiyo kujadiliana jinsi ya sekta ya mabadiliko ya tabia
nchi itakapoingizwa katika mpango wa halmashauri na bajeti za halmashauri
katika ngazi ya vijiji na wilaya.
Awali akifungua semina hiyo mkurugenzi wa Halmashauri ya
Meru Bakari Salim amewataka wananchi
kuachana na biashara za kukata miti
pamoja na kuchoma mikaa kwani hiyo yote ni uharibifu wa mazingira.
Baadhi ya madiwani walioodhuria katika Semina hiyo akiwemo
diwani wa kata ya Makiba Emannuel Pendael Molel
wamesema kuwa wataenda kuwa chachu katika kata zao kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa
mazingira.
No comments:
Post a Comment