Serikali
yatakiwa kuweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali.
Na fredy salvatory
Serikali imetakiwa kuweka mazingira rafiki kwa wananchi wote
wanaojishugulisha na biashara ndogo
ndogo maarufu kama ujasirimali ili kuwafanya kuwa na wigo mpana wa kuweza kukubaliana na hali ya maisha
pamoja na kuchagia katika shughuli za kimaendeleo.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na baadhi ya wanawake ambao
wanajishugulisha na biashara ndogondogo ya kulima nakuuza mbonga za majani
maarufu kama wajasiriamali jijini Arusha katika mahojiano na blog hii.
Walisema licha ya kujenga mazingira mazuri ya kufanya
biashara lakini wanatakiwa kuangaliwa
kwa upande wa mikopo itawezesha kupanua na kukuza biashara yako na kujikimu
kimaisha na kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi ‘Tunaiomba serikali
kuhakikisha inatuwekea mazingira kwa watu tunao jishughulisha hizi ndogondogo
pamoja nashughuli zote za ujasiliamali
kwani inatusaidia kuondokana na wimbi la
umasikini pia tutakuwa na wasaa
wakuchangia michango katika shughuli za kimaendeleo’ alise moja ya mwana mama mjasiriamali aliejitambulisha kwa jina la Mama Rehema.
Alisema wakiwekewa mazingira mazuri na rafiki katika
serikali wataweza kujiajiri wenyewe na
kuondoa dhana ya kusubili
kuajiriwa na mtu au kuajiriwa na serikali huku wakiwataka wanawake wote kuwaiga
wao kwa kujishughulisha na shughuli
mbalimbali ili kuziendeleza familia zao na kutokuwa tegemezi alisema mama huyo
na kuongeza kuwa kwasasa imepita miaka kumi (10) toka aanze kufanya biashara
hiyo huku akidai kupitia biashara yake hiyo anasomesha watoto wake wawili mmoja
akiwa katika shule ya sekondari na mwingine akiwa katika
shule ya msingi.
Aidha mama huyo alisema kuwa kipindi hiki serikali iweze kuwawekea hata maeneo ya
kufanyia biashara pasipo kukimbizwa na
kuwakosesha amani wawapo katika biashara na kuwaasa wanawake kujitambua na
kuwataka kuungana kuwa na vikundi vitakavyo
wasaidia kukuza miladi yao na kuwa namichango kwaajili ya kuendeleza
miladi yao.Nakusema kuwa mkiwa na vikundi wanawake mnakuwa sitegemezi katika familia
naendapo mtu akitaka kufanya mladi
huunmganisha mawazo na kujiendereza kimaisha na katika kuinua uchumi wa familia
na nchi jumla.
No comments:
Post a Comment