Friday, April 22, 2016

IFAHAMU ASALI KAMA TIBA NA SIYO ZAO. 


Makala haya yameandaliwa na John Billah 

Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza ukajiuliza maswali mengi ya msingi ni kwa nini nimeamua kuandika makala yenye kichwa cha habari kama hiki kwa siku a leo,lakini jibu la msingi yamkini waweza kuwa ni mmojawapo ya watu wanaoichukulia asali kama ni sehemu ya kiburudisho katika matumizi yao ya kila siku ,ikiwa ni pamoja na kuilamba ,kuitumia kwenye uji kama sukari mbadala kwa kinywaji.

La hasha ndugu mpenzi msomaji wa makala hii napenda kukukaribisha katika safu hii ya makala mahsusi iliyojikita katika Suala zima la zao la asali pamoja na faida zake katika maisha ya mwanadamu yenye kila aina ya nakshi hapa duniani .

Asali ni zao mojawapo linalotengenezwa na mdudu fundi anayejulikana kwa jina la Nyuki kwa kutumia vitu kadha wa kadha kama vile maua ,mbegu za miti,ua za matunda mbalimbali,mbarawa ikiwemo vitu vyenye asili ya chumvi pamoja na vitu vyenye asili ya majimaji ili kuunda asali ambayo leo hii mimi na wewe tunaitumia kwa matumizi .

Na pia asali hii imeweza kugawanywa katika makundi makuu mawili na wataalamu mbalimbali wahusuyo mambo ya nyuki na asali,mbayo kundi la kwanza ni asali inayo tengenezwa na vyanzo vya nyuki wenyewe kutoka porini aidha kuiandaa katika mapango ,magome ya miti,pamoja na mizinga ya kuchongwa na mwanadamu ambayo huianika kwa taraji la nyuki kupata hifadhi kwa ajili ya kutengeneza asali katika sehemu hizo husika.


Pia kundi la pili ambalo wataalam wamefafanua ni ile asali ambayo hupatikana kwa njia ya kuandaa masanduku mahsusi ,maboksi pamoja na mizinga y kuchongwa na watu binafsi,makampuni ,taasis ,na mashirika au miradi ya ufugaji nyuki na kwenda kuianika sehemu ambazo ni shawishi kwa ajili ya makazi ya wadudu nyuki ili waweze kutengeneza asali ambayo kwa kitaalam tunaita ni asali ya nyuki ya kufugwa kutokana na elimu  ya ufugaji nyuki.

Mbali ya mimi na wewe kuitumia asali kama sehemu ya kiburudisho ,ukweli ni kwamba asali ni zao pekee duniani kama chakula chenye kukaa muda mrefu pasipo kuharibika au kuoza kwa haraka pasipo kujali ni wapi zao hili limehifadhiwa kwa matumizi ya kila siku.

Asali licha ya kuwa ni rafiki wa karibu kwa maisha ya mwanadam ,tambua asali ni mojawapo ya tiba murua kwa huduma ya awali kwa mhanga wa ajali yeyote wa majeraha ya moto,hutumika kumpaka ili kupunguza maumivu makali katika jeraha la mtu aliyeungua moto maana huvuta maumivu makali ya moto kwa asilimia 55 hadi asilimia 90.kabla ya kumuona daktari kwa ajili ya tiba kwa kina.

Pia asali hutumika kama dawa ya kikohozi kwa mtu yeyote anayepitia adha ya ukavu wa kikohozi kigumu wakati wa kukohoa ,maana asali huchanganywa na yai bichi na ndipo mgonjwa akipatiwa inakuwa ni tiba tosha kwa kuuondoa kikohozi kigumu au kwa mtu ambaye sauti yake ipo chini sana kwa ajili ya kukohoa muda mrefu.


Kwa tamaduni ya jamii ya watu waishio maeneo ya vijijini hupenda kuitumia asali kama sehemu kuu ya matumizi kwa ajili ya kuandaaa kifungua kinywa ikiwa ni pamoja na kuitumia katika uji kama sukari mbadala,kuipaka kwenye mikate ,na kubwa zaidi huitumia asali katika matumizi ya kinywaji aina ya pombe ya kienyeji ili kuongeza makali ya pombe iweze kuwa na kilevi kikali zaidi.

Na sanjari na hapo mwanadamu anashauriwa kila siku iendayo kwa Mungu awe anapata angalau kijiko kimoja cha asali ili kuweza kmpungumzia maradhi mbali mbali yaliyopo ndani ya mwili wake ikiwa ni pamoja na kusafiha mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuratibu kiwango cha sukari mwilini.

Naam mpenzi msomaji wa safuu hii ya makala kuhusu zao la asali kwa leo tukomee hapa ,chukua hatua thubutu kwa kuitumia asali kila siku na uwe nayo ndani ya nyumba yako kama rafiki wa afya wa karibu ,maana siku zote mchawi wa maisha yako ni wewe binafsi……,tukutane wakati ujao upate kujua zao hili linapatikana wapi hapa Tanzania?????.

No comments:

Post a Comment