Sunday, May 1, 2016

MATATIZO YA KISAIKOLOJIA
Na fredy salvatory
makala na chanzo cha  gazeti
Kukubali na Kukabili matatizo ya Kisaikolojia
     
  Matatizo ya kisaikolojia ni nini?
   Matatizo ya kisaikolojia ni yale yanayoathiri ufahamu wa mtu na uwezo wake wa kufikiri,kupambanua mambo au kufanya uamuzi katika shughuli zake za kila siku.Matatizo ya kisaikolojia huweza kutokea katika hatua yoyote ya maisha ya binadamu kuanzia utoto hadi uzee.Matatizo ya kisaikolojiaa huweza kusababishwa na mambo mengi.Baadhi ya mambo hayo ni
1.     Ukosefu wa chakula bora.Chakula bora huwa na virutubisho,kama vile madini na vitamini ambavyo huimarisha afya ya ubongo na kutafanya tuwe na hali ya utulivu kiakili
2.     Ubongo kukosa damu ya kutosha ambayo husambaza virutubisho,oksijeni,na kuondoa kabonidayoksaidi,hivyo kuufanya kushindwa kufanya kazi ipasavyo
3.     Majeraha kichwani yanayotokana na ajali
4.     Kupotea mtu unayempenda au unayemtegemea,kwa mfano kufiwa na mzazi/wazazi,walezi  au ndugu wa karibu
5.     Tukio la kuumiza au kusikitisha kwa mfano kufeli mtihani,kubakwa,kuibiwa mali,kuteswa au kugundua kuwa una ugonjwa usionatiba
6.     Kuvunjika kwa ndoa hivyo watoto kukosa msimamo na mashauri au msimamizi
7.     Ugomvi kati ya wazazi
8.     Kutelekezwa
9.     Mazingira yasiyo salama kwa mfano vita na majanga ya asili kama vile mafuriko,kimbunga na milipuko ya volcano.
10.         Utumiaji wa dawa za kulevya.                                            Matatizo ya kisaikolojia huweza kuleta madhara mengi,yakiwemo kupata ulemavu,shinikizo la damu,maumivu  ya mwili,kushindwa kusoma au kufanya kazi,kukosa marafiki,kukosa furaha na amani au hata kupoteza maisha.
Dalili za mtu mwenye matatizo ya kisaikolojia.   
·       Kuwa na hasira inayopindukia
·       Kuhamaki kwa mambo madogo na hata ya kawaida
·       Kuwa na huzuni na kujiona huna thamani kwa jamii
·       Kuchanganyikiwa na kukosa usikivu au umakini
·       Kujitenga na wengine na kushidwa kujenga uhusiano,kwa mfano kuwa na marafiki
·       Kuwa na wasiwasi na uoga uliopindukia mara kwa mara
·       Kukosa usingizi na kuweweseka wakati ukiupata
Aina za matatizo ya kisaikolojia.
         Kuna aina mbalimbali za matatizo ya kisaikolojia.Baadhi ya aina hizo ni wasiswasi,mafadhaiko na utukutu
MATATIZO YA KUWA NA WASIWASI
Wasiwasi ni jambo la kawaida kwa mwanadamu.Hata hivyo kuna wakati mtu huwa na wasiwasi na hofu kuliko kawaida hata kwa vitu ambavyo ni vya kawaida hata kwa vitu ambavyo na vya kawaida sana au vitu ambavyo havipo kabisa.Inapofikia hali hiyo,tunaweza sema mhusika ana ugonjwa wa wasiwasi.
Dalili za ugonjwa wa wasiwasi
1.     Kuogopa vitu vya kawaida kama vile wanyama ,(mbwa,nyoka,au mende),kupanda majengo marefu,au kuogopa kukaa kwenye chumba cha pekee yako au kwenye lifti
2.     Aibu isiyo kuwa ya kawaida
3.     Kushindwa kutulia
4.     Kukosa usingizi
5.     Kuhisi kizunguzungu na kutokwa jasho

 UGONJWA WA MAFADHAIKO
Mfadhaiko ni tatizola kisaikolojia linalotokana na msongo wa mawazo kutokana  na tukio la kuhuzunisha,kama vile kufiwa,kufeli mitihani,kukataliwa,kutelekezwa na mme/mke.Kwa kawaida watu hupatwa na huzuni kutokana na matukio ya kusikitisha na hurejea katika hali yao ya kawaida baada ya muda.Hata hivyo watu wenye mafadhaiko hushindwa kukubali hali yao ya kawaida baada ya muda.



               Dalili za mtu mwenye mafadhaiko
·       Uchovu
·       Kuhisi upweke na kujiona huna thamani hata kutamani au kujaribu kabisa kujiua
·       Kutotamani kufanya kitu chochote, hata kazi au mambo ambayo ulikua unayapenda.Watoto huwa hawapendi kucheza au kufanya kazi za shule
·       Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.Baadhi ya watu huweza kula sna kuliko kawaida
·       Kushidwa kufukiri, kutokua  kuwa makini na kufanya uamuzinjuu ya mambo ya maisha yake ya kila siku
·       Kushindwa kupata usingizi lakini  baadhi hulala kuliko kawaida
·       Kujiona kuwa  ni mbaya na huwezi kufanya kiyu chochote kizuri chenye manufaa


 TATIZO LA UTUKUTU                                      
Kwa kawaida watoto ni watundu.Utukutu ni utundu usio wa kawaida ambao muda wote mtoto hushidwa kutulia na hata kufanya vitendo vya hatari au uharibifu.Baadhi ya wtoto wenye tatizo hili la utukutu,hulazimika kupelekwa hata jela ya watoto ambako hupewa mafunzo maalumu ili waweze kuishi maisha ya kawaida.Kukubali na kukabili matatizo ya kisaikolojia ni muhimu kudhibitiwa,huathiri afya zetu,mihemko,uhusiano  na wengine,uzalishaji mali,maisha kwa ujumla na hata kusababisha matatizo kwenye familia.Matatizo ya kisaikolojia yanaweza kudhibitiwa na mtu kuendelea na maisha yake kama kawaida.Matatizo kutafita n ya kisaikolojia  kudhibitiwa na mtu kuendelea na maisha yake kama kawaida.Matatizo hayo ni kukubali tatizo na kuwa tayari kukubaliana nalo.Zifuatazo ni baadhi ya njia za kukubaliana na matatizo ya kisaikolojia
·       Kukubaliana na hali halisi ingawa umepata tatizo inabidi kutafuta njia sahihi ya kuondoa na kulisahau tatizo hio
·       Epuka kujitenga bali shirikiana na kuchanganyika na watu.Hii husaidia kupunguza huzuni au mihemko
·       Omba msaada au ushauri kutoka kwa watu wa karibu au unaowaamini,kwa  mfanorafiki,ndugu,mshauri nasaha au kiongozi wa dini.Waeleze jinsi unavojisikia na fanyia kazi mashauri yao
·       Jiwekee ratiba ya kila siku na uitekeleze,usipote mda kwa kukaa bure
·       Fanya mazoezi,pata usingizi wa kutosha na muda wa kupumzika pamoja na muda wa kusirikiana na watu katika shughuli za kijamii
·       Imarisha afya yako kwa kula chakula bora,epuka ulevi na dawa za kulevya kwani huongeza ukubwa wa tatizo

·       Waone wanasaikolojia

No comments:

Post a Comment