Tuesday, May 3, 2016

YANGA AFRICAN'S LEO 3 MAY 2016 INAYO TALAJIA KUCHEZA  NA WANA WASHINYANGA STAND UNITED,YANGA IKIWA UGENINI
chanzo na habari leo
VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga leo watakuwa wenyeji wa Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo wakitokea Jijini Mwanza, ambapo Jumamosi iliyopita iliifunga Toto Africans na kujiimarisha kileleni kwa kufikisha pointi 65, wakati wenyeji wao Stand siku hiyo walikubali kipigo cha mabao 2-1, kutoka kwa Mwadui FC, mchezo uliopigwa Uwanja wa Mwadui Complex.
Yanga tayari wametua mkoani Shinyanga tangu Jumapili kujiandaa na mchezo huo huku wakiwa wamepania kupata pointi tatu ambazo zitazidi kuwaweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao msimu huu ambao unashirikisha timu 16.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani Stand United inayoshika nafasi ya saba kwenye msimamo na pointi zao 34, hawatakubali kupoteza mchezo mwingine tena wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Kocha wa Stand United, Mfaransa Patrick Liewig, alisema amekiandaa vizuri kikosi chake kwa ajili ya kushinda mchezo huo ambao utawasaidia kumaliza msimu kwenye nafasi nzuri zaidi kuliko waliyo sasa.
Liewig alisema anajua anakwenda kupambana na timu ngumu inayoongoza ligi lakini wamejipanga kuhakikisha wanacheza vizuri na kushinda kutokana na maandalizi waliyoyafanya mara baada ya kumalizika mchezo wao uliopita dhidi ya Mwadui FC.
Katika mchezo huo, kocha Liewig atakuwa akiwategemea zaidi wachezaji wake Elias Maguli, kiungo Amri Kiemba na Haruna Changongo ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chake huku safu ya ulinzi ikiwa chini ya Nassor Masoud ‘Chollo’ , Abuu Ubwa na Rajabu Zahiri.
Kwa upande wake kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, alisema amekwenda Shinyanga kwa ajili ya pointi tatu na ana uhakika wa kuzipata kutokana na uimara wa kikosi chake ambacho kimekuwa kikiimarika katika kila mechi wanayocheza hivi sasa.
Pluijm alisema anaiheshimu Stand United kuwa ni moja ya timu nzuri na ngumu ambayo inaundwa na wachezaji wengi wazoefu, lakini anajivunia ubora wa wachezaji wake ambao ushiriki wao katika michuano ya kimataifa umewapa uzofu mkubwa na ndiyo sababu ya matokeo ya ushindi wanao upata.
Pluijm alisema kikosi chake cha leo hakitakuwa na mabadiliko makubwa sana tofauti na kile kilichoanza kwenye mchezo ulipita dhidi ya Toto Africans, ambapo katika safu ya ushambuliaji akiendelea kuwatumia mapacha wawili Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao wote kwa pamoja wamefunga mabao 33.

No comments:

Post a Comment