CHACKYI YA JIJINI ARUSHA YAZIDI
KUWANG’ALISHA MASHABIKI WAKE LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA KATIKA
UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID
Arusha.
30.03.2016.
Na Fredy salvatory.
Michuano ya ligi daranja la tatu ngazi ya mkoa wa Arusha
kumtafuta bingwa wa mkoa kwa ajili ya kushiriki ligi daraja la pili Tanzania
bara imeendelea kutimua vumbi ambapo hapo jana katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha .
Katika mchezo uliochezwa jana ulizikutanisha klabu ya Charky
inashika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 10 kibindoni dhidi
ya klabu ya Monacti fc wanaoshika nafasi ya nne
wakiwa tayari wameshajikusanyia
pointi nne .
Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute kutokana na kila
timu kuhitaji kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutoa
ubingwa ulimalizika kwa klabu ya Chakyi kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya
wapinzani wao klabu ya Monacti ambao hawakuambulia chochote katika mchezo huo.
wakienda mapumziko kipindi cha kwanza chackyi wakiongza magori mawili 2-ya kipindi hicho cha kwanza cha mchezo
Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Chakyi Rashidi
Chama alizungumzia mchezo huo na
kusema timu yake imejipanga vizuri na
anamatumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa siku ya jumamosi na pia alisema
tatizo la timu nyingi kujitoa katika mashindano inasababishwa na kuwa na
viongozi ambao sio wanamichezo.
Kwa upande wake
katibu wa mashindano hayo kwa mkoa wa Arusha
Maki Warioba alisema kuwa timu ambazo zilikuwa zinashiriki katika
mashindano hayo ni nane na baadae timu moja kujiondoa katika ligi hiyo baada ya
kushindwa kucheza mchezo mmoja ambayo ni Arusha Meet mpaka sasa zimebakia timu saba.
Matokeo hayo yalionekana kuinufaisha club ya Chackyi ambayo
iliweza kufikisha point 10 nyuma ya vinara wa ligi hiyo ambao ni club ya pepsi
ambao tayari walijikusanyia point 13 katika ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.
No comments:
Post a Comment