LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA ARUSHA HATIMAE IMEFIKA KI LELENI
03/04/2016
Michuano iliyokuwa ikiendelea jijini Arusha ya
ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa ambapo jioni ya leo imezikutanisha timu nne,
mbili zikiwa zimegongana pointi, timu hizo zilizo kipiga katika viwanja viwili tofauti moja ikichezea
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid na mchezo mwingine ukichezwa kwenye uwanja
wa Iliboru.
Katika mchezo
uliochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid umezikutanisha timu ya Karatu United na
timu ya Nyota Fc,Mtanange huo ulikuwa wavuta nikuvute kila timu ikitaka kuibuka
na ushindi ambapo timu ya Karatu ilipo wazidi ujanja wapinzani wao na kujipatia
goli moja 1-0 kupitia kiungo mshambuliaji John Thomas John ambaye amewapatia
goli hilo lilodumu hadi dakika 90 za mchezo
huo.
Kocha wa
timu ya Karatu amesema walichokuwa
wanakitaka ni kuweka heshima ya Karatu united mchezo huo ulikuwa muhimu kwao
kuliko michezo mingine nakuwaomba wadau wa karatu united kujitokeza kusaidia timu hiyo ili katika
msimu ujao iweze kufanya vizuri katika mashindano ya ligi ngazi ya mkoa
Vilevile
amewaasa viongozi wa mpira kuwa waungwana hasa waamuzi wawapo uwanjani kwani
timu zinatumia gharama nyingi kwa ajili ya mashindano na pindi wanapo panga
matokeo inakatisha tama timu shiriki.
PICHA
WACHEZAJI WA KARATU UTD
Katika
mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Ilbolu ambao uilikuwa unafuatiwa na
washabiki wengi ulikuwa kati ya klabu ya Pepsi na klabu ya Chakyi fc uleweza
kumalizika kwa klabu ya Pepsi fc kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kufanikiwa
kutoa ubingwa wa mkoa wa Arusha baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 16 katika
ligi hiyo
No comments:
Post a Comment