Tuesday, May 2, 2017

FAHAMU Aina 12 Ya Wanawake Ambao Watayafanya Maisha Yako Kuwa Magumu

Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.

Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani...nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

9. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

10. Asi na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

11. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

12. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua

Monday, April 17, 2017

Usidharau..Kabla ya Kufunga Ndoa au Kusexy KavuKavu na Mpenzi Wako Hakikisha Mmepima Haya Magonjwa 4 ya Kuambukizwa

1. Ugonjwa wa kaswende.
Kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu. Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiana huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri. 

Kidonda hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kua kichaa.
  
2. Ugonjwa wa hepatitis B.
Ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi. 

Ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu, Mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa hii mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.

3. Ugonjwa wa ukimwi.
Huu ni ugonjwa unaofahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya Radio, Tv, Magazeti na sehemu mbalimbali.

Ugonjwa huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga. 

4. Ugonjwa wa gonorea.
Huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani Wanaume na Wanawake, mara nyingi Mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwana mke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. Mwishoni ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba

Saturday, April 15, 2017

Music wa dini kwaya vijana

https://youtu.be/4DKs-fGgSW4

Mbinu za kumchokoza mpenzi wako au mwanamke kihisia



Je una ndoto ya kutaka kuwa na nguvu ambazo zitaweza kuwafanya wanawake wakuandame na kukupigania kila wakati? Ijapokuwa hii inaweza kuwa ndoto kwa wanaume wengi kule nje, wanaume wengi wanadhania kuwa jambo kama hili haliwezekani katika maisha ya kawaida kama hauna umbo la kuvutia ama pesa za kuwahonga wanawake. Huu hauna ukweli wowote.

Kupata wanawake wakuandame mara kwa mara ni ndoto ya kila mwanaume. Na ni haki yako ya kujua kutimiza jambo hili.

Ukiwa unajua mbinu za hakika za kutumia wakati unapotongoza, unaweza kumfanya mwanamke wa ndotoni mwako afanye chochote unachotaka wewe kwa kumuagiza kwa upole – aminia hili. Kama team ya Nesi Mapenzi, tumekuandalia hili chapisho kuelieza mbinu hii ili uzingatie yale muhimu ya kutimiza.

#1 Jenga taharuki
Kama unamtaka mwanamke afuate sheria zako, unahitajika kujenga utangulizi. Wanawake wanapenda drama na taharuki, hivyo basi endelea kuwapatia hayo, watakuwa kila wakati wakikuandama kutaka zaidi. Mwanzo kadri unapoendeleza taharuki na vituko katika maisha yako, ndivyo watataka zaidi kujihusisha katika maisha yako. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini kuna baadhi ya wanawake huwa wanapenda kujihusisha na mwanaume mmoja ambaye ana wanawake wengi? Huwa kwa kawaida mwanaume kama huyu huwa amewaunganisha wanawake hawa kwa kuwakeep busy na vioja na drama za mara kwa mara.

#2 Cheza mchezo wa kutoelewa
Kitu kingine cha kufanya kuhakikisha kuwa wanawake hawatakutoka katika akili zao ni kwa kuwafanya wanawake wasijihisi huru/comfortable wakiwa na wewe. Kama mwanamke atahisi kuwa hahitaji kutumia bidii zake ili kupata atenshen kutoka kwako, basi atapoteza interest na wewe baada ya muda mfupi. Kwa jambo hili utakuwa na uhakika mkuu ya kuwa utapoteza interest ya mwanamke haraka sana, kama atagundua kuwa unasomeka kirahisi. Kwa kukabiliana na hili tatizo, hakikisha kuwa unampatia mwanamke wakati mgumu wa kukuelewa. Hii unaweza kuitimiza kwa kumchanganya, kumtia wasiwasi, mchezee akili nk ilimradi tu asipate kukuelewa ajenda au mambo yako kiurahisi. Kumchezea mchezo wa kutoeleweka kutakufanya uicontrol akili yake vile unavyotaka wewe.

#3 Cheza drama
Kama tulivyotangulia kusema awali kuwa lazima uwe na drama katika maisha yako. Wanawake hupenda drama katika maisha yao. Ushawahi kujiuliza kwa nini wanawake wanapenda kuangalia tamthilia au soaps za Mexico? Ni kwa sababu wanapenda na kutamani maisha yao yawe na drama za mara kwa mara. Bila drama katika mahusiano yako na mwanamke utamfanya aboeke na kupoteza interest katika mahusiano yenu. Hivyo basi kama utajenga drama ambayo mpenzi wako amekuwa akitamani umfanyie, basi atapendezwa na wewe na itakuwa vigumu kwake kuingiwa na akili za kuwa amechoshwa katika uhusiano wenu.

#4 Tumia mbinu za kisaikolojia
Mbinu za kisaikolojia huwa hufanya kazi kubwa sana ikija katika swala la kumtongozo na kumzuzua mwanamke. Mbinu hizi humrahishia kazi mwanaume pakubwa sana wakati anaaproach ama kumtongoza mwanamke. Haijalishi kama ndio unaanza kutongoza ama wewe ni bingwa, mbinu hizi za kisaikolojia hufanya kazi nyakati zote. Mwanzo kuna mbinu nyingine za kisaikolojia ambazo unaweza kujua kile ambacho mwanamke anafikiria akilini mwake na jinsi ya kukabiliana na vile anavyofikiria ili utumie kwa manufaa yako wewe mwenyewe.

#5 Ivumbue formula ambayo inawekwa siri ikija katika kutongoza
Ukweli usemwe. Kuingia katika akili ya mwanamke na kuijeuza fikra yake ya kumfanya akuone kuwa wewe unavutia ni kazi rahisi ya kufanya. Kile ambacho unahitajika kufanya ni kutafuta ile formula ambayo itafanya kazi kwako na kukupatia nguvu za kuweza kumpata yule mwanamke ambaye amekuwa akizunguka katika akili yako kwa muda huo wote. Ukishaipata hio formula yako, unaweza kuwajeuza wanawake vile unavyotaka wewe, bila kuangalia ushupavu wako katika dunia ya kudeti wanawake. Kufanya kuwa huwatambui huwa inafanya kazi kila wakati! Morrissey katika mtandao wa Hubpages alisema kuwa “Kadri unavyozidi kunipuuza ndivyo ninavyozidi kujisogeza karibu yako.” Hii ni kweli katika maisha ya mwanamke. Mwanamke unapomuonyesha kuwa umepoteza interest na yeye atafanya juu chini kuhakikisha kuwa atarudisha interest...

Upo!? Kazi kwako

Thursday, April 13, 2017

Jinsi ya kushawishi wanawake utokenao out

Kabla hujaendelea kusoma chapisho hili, nataka ufahamu ya kwamba kuna njia moja pekee ya uhakika ambayo unaweza kuitumia kuepuka kukataliwa na wanawake katika dunia na miaka ya kisasa, nayo ni kukaa nyumbani na kuepuka kutangamana na wanawake kabisa. Naturally hakuna shangwe kwa hilo, so unapaswa kukubali kuwa kukataliwa kunakuja wakati ambapo utaamua kuapproach mwanamke. Njia nzuri ya kueleza tatizo hili ni kwa kukabiliana nalo mzima mzima. Mwishowe, kadri unavyozidi kufanya mazoezi ndipo utakapozidi kuwa na mafanikio katika kuapproach wanawake na kuwashawishi watoke out na wewe.

Hizi hapa ni mbinu tofauti tofauti ambazo unaweza kuzitumia kuwashawishi wanawake watoke out na wewe na kuepuka kukataliwa na mwanamke kwa namna yeyote ile.

#1 Makinika na timing yako
Hata kama wewe unavutia ama kupendeza mbele ya wanawake kiasi gani, hutoweza kuwa na wakati rahisi wa kumfanya mwanamke avutiwe ama umfanye akubali kutoka out na wewe kama hujua vile timing inavyofanya kazi. So, utawezaje kufanya timing yako iwe bora? Utajuaje kama ni wakati muruwa wa kumuapproach mwanamke kwa mara ya kwanza na kumtongoza? Unaanzishaje gumzo na mwanamke? Well, kwa wale ambao ndio wanaanza kujua maswala ya kudeti, unahitajika kwanza kujua jinsi ya kusoma vile miondoko ya mwanamke hufanya kazi. Baada ya hapo, unaanza kutafuta ishara hakika ambazo zitakwambia kuwa mwanamke fulani yuko tayari kuapproachiwa na kutongozwa. Kama mwanamke hataonyesha dalili ama ishara zozote, basi unaachana naye na kutafuta windo jingine.

#2 Mhusishe katika gumzo la kisawasawa
Kama unataka mwanamke atoke out na wewe, basi unapaswa kumfanya afall in love na wewe kila dakika ambayo utakuwa unaspend na yeye. Kufanya hivi, unapaswa kuanza na lengo katika akili yako kila wakati ambapo utaamua kumuapproach mwanamke. Jiambie mwenyewe kuwa siku hii utamfagia mwanamke kutoka miguuni mwake. Jiambie mwenyewe kuwa unaweza kumfanya huyu mwanamke ajihisi kama wewe ni nusu wa moyo wake. Hii inaweza kuonekana kazi ngumu kwa sasa, lakini si lazima iwe hivi. Unaweza tu kujiweka ama kujifananisha wewe kama  mwanaume asiyejulikana na ambaye amebobea katika maswala ya kutongoza, na hakika kwa wale wanawake ambao watakutana na wewe siku hio watakuchukulia kama wewe ni mwanaume bora ambaye wameweza kukutana naye.

#3 Ipaze tenshen ya mapenzi
Kitu kingine ambacho unapaswa kufanya ni kumfanya mwanamke apandwe na tenshen ya mapenzi kila wakati anapokuona – tenshen ya hali ya juu ambayo itamfanya aitikie kila kitu ambacho utamuamuru kufanya. Kemia ya kimapenzi ambayo inafanya kazi kama mzizi, ambayo unaweza kumfanya mwanamke arushe mbali wasiwasi wake wote ambao anaweza kuwa anauhisi na kumfanya afanye kila kitu ambacho unataka wewe. Pindi utakapofanikiwa kuongeza level yake ya tenshen za kimapenzi, hutapata shida kwa kueneleza ajenda zako vile unavyokusudia wewe

Wednesday, April 12, 2017

Sababu zinazoweza kuchangia hedh yako kuchelewa

Sababu 5 zinazoweza Kuchangia Hedhi yako Kuchelewa Kuiona


Wasichana wengi huanza kutawaliwa na hofu kila wanapoona wakati wa kuonda siku zao (hedhi) umefika halafu hawaoni hali ikijitokeza.

Wengi wanapoona hali hiyo mawazo yao yote hueleka kuwa wameshashika ujauzito, lakini kumbe hali hiyo huweza kutokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo hizi hapa 5 chini;-

1. Huweza kuwa ni mabadiliko ya homoni mwilini

2. Mabadiliko ya uzito wa mwili

3. Msongo wa mawazo

4. Mpangilio au mabadiliko ya mlo

5. Maambukizi kwenye via vya uzazi

Tuesday, April 11, 2017

Tabia za madem wapenda pesa

1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima.
Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa Sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao.

Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine kubwa wakati akiwa bado na simu mpya.

Katika maisha ni bora uingie jehanam kuliko kukutana na mwanamke mpenda pesa kwani utateseka Sana kwa ajili yake na bado hata ona msaada wako.

Sio rahisi kujenga familia bora na mwanamke mpenda pesa.

2. Wengi hutoka familia masikini.
Wanawake wengi Kama sio wote ambao hupenda pesa kuliko utu wao hutoka familia kame Sana. Ukame wa kiuchumi mpaka kiakili. Wengi wao huweza kutoa hata rushwa ya ngono ili tuu wapate pesa wasijue miili yao inathamani zaidi ya zile karatasi.

Mtu ni masikini unandoto za kuwa na mwanaume mwenye pesa nani alikuambia wenye pesa wanataka masikini.

Umasikini wako usikufanye ujidharau au mtu akudharau. Lipo kundi dogo la wanawake wanaojitahidi kutetea thamani ya jinsia yao lakini wengi wao ni wakuonewa huruma tuu.

3. Wengi wao hawana elimu ya kutosha.
Mwanamke aliesoma akaelimika hawezi hangaika na pesa ya mtu. Ndio maana wanawake wachache huhangaika kwajili ya kujitegemea na sio kumtegemea mwanaume.

Wanawake wengi wenye elimu na vipato vizuri huwezi msikie akiongelea pesa Kama kigezo muhimu kwa mwanaume anayemuhitaji awe mume wake.

4. Ni wavivu na wasio na mawazo.
Wanawake wote wanaopenda pesa ni wavivu kupita kiasi. Uvivu wao umeanzia akilini kiasi kwamba hawana mawazo ya maendelo. Utakuta mwanamke anawaza mambo mepesi kabisa Kama urembo, nguo, mtoko, n.k.

Wanawake wapenda pesa ni hatari kwa ustawi wa familia.
Huwezi kuwa na familia kubwa ukiingia katika bahari ya viumbe hawa.

5. Hawana shukrani wala uvumilivu.
Wanawake wapenda pesa huwezi msikia akikushukuru zaidi ya kujichekesha tuu na kubinua makalio.

Kwa mfano amekuomba milioni moja then ukampa laki tano basi utamsikia akisema sasa hii nitafanyia nini, au niongezee tena mume wangu huku akikushika kifua au ndevu.

Wanawake wenye hekima hushukuru mpaka mwanaume anasikia aibu.

Suala la uvumilivu halipo kwa hawa wanawake. Shida ikitokea ukishindwa kuitatua kwa wakati huo basi hesabu umeliwa. Yaani kwao kukusaliti ni jambo lisilo na mashaka.

Mafanikio ya kweli acha kulalamika

Ukitaka Mafanikio Ya Kweli Acha Kulalamika Juu Ya Mambo Haya....!!! http://www.udakuspecially.com/2017/04/ukitaka-mafanikio-ya-kweli-acha.html

Tuesday, September 27, 2016

DOWNLOAD VIDEO: Tox Star Ft. Barnaba – ChillaxDOWNLOAD HERE

                                                    Tokeo la picha la DOWNLOAD VIDEO: Tox Star Ft. Barnaba – Chillax
DOWNLOAD VIDEO: Diamond Platnumz ft Raymond - Salome ( Traditional)DOWNLOAD HERE 
                                             Tokeo la picha la SALOME BY DIAMOND

MADEMU WA USWAZI WAMUIMBISHA MCHINA KISINGELI DUH HAHAHA JIONEE KITUKO M...

Monday, May 23, 2016


 VAN GAAL AMFUATA STWART HALL WA AZAM FC 


 Manchester United imemtimua kazi kocha wake Louis van Gaal siku mbili tu baada ya kutwaa taji la FA Cup Jumamosi iliyopita kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace. Van Gaal ametimuliwa kufuatia mwenendo wake mbovu kwenye Premier League na nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho. Benchi lake la ufundi la Waholanzi wenzake Albert Stuivenberg na kocha wa makipa Frans Hoek nao pia wamefungashiwa virago.





                                                          kocha wa zamani wa man u Louis van Gaal

 Ed Woodward aliwasili kwenye ngome ya mazoezi ya Manchester United - Carrington training complex kwaajili ya maongezi na Van Gaal Jumatatu asubuhi kabla ya muda mfupi baadae kutangaza kuwa kocha huyo ametimuliwa.  Mourinho anatarajiwa kuwa na maongezi ya mwisho na Manchester United Jumanne kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitatu huku wasaidizi wake  Rui Faria na kocha wa makipa  Silvino Louro nao wakitarajiwa kumfuata Old Trafford. Hatma ya kocha msaidizi Ryan Giggs bado iko inaelea hewani ingawa kuna kuna habari zinazodai kuwa Mourinho bado angependelea kuwa naye. Louis van Gaal amefukuzwa kazi Manchester United  Van Gaal akiwasili kwenye uwanja wa mazoezi muda mfupi kabla hajatimuliwa

Sunday, May 22, 2016


Ukisikia mtu mfupi kuliko wote duniani basi huyu mwanaume wa nchini Nepal atakuwa amevunja rekodi ya dunia, ana urefu wa sentimeta 56 na uzito wa kilo 12 tu.


NewsImages/6229370.jpg
Chandra Bahadur Dangi akiwa amesimama wima kuonyesha urefu wake wa sentimita 56 tu




Maafisa wa kitabu cha rekodi za dunia, Guinness World Records wanatarajiwa kusafiri kwenda nchini Nepal kukutana na mtu mfupi kuliko watu wote wafupi waliowahi kuishi duniani.

Babu mwenye umri wa miaka 72, Chandra Bahadur Dangi ana urefu wa sentimita 56 na uzito wa kilo 12 tu na anaishi kwenye kijiji kilichopo kwenye mabonde yaliyopo kusini magharibi mwa Nepal.

Kwa miaka mingi babu Chabdra amekuwa akiishi kwenye kijiji hicho akijipatia umaarufu kwa ufupi wake hadi hivi karibuni televisheni ya taifa ya Nepal ilipomuonyesha na kumpima urefu kucheki kama amevunja rekodi ya dunia.

Kugundulika kwa Chandra kuwa ni mfupi kuliko watu wote duniani kumemfanya Chandra ajipatie umaarufu wa ghafla nchini Nepal na duniani.

"Tunaenda Nepal kwenye kijiji cha Chandra ili kuthibitisha urefu wake na kumtangaza rasmi kuwa mtu mfupi kuliko wote duniani", alisema afisa wa Guiness worldrecords, Craig Glenday.

Ndugu wa Chandra walisema kuwa Chandra ana afya njema hajawahi kuugua wala kwenda hospitali na hatumii dawa zozote.

Kwa hivi sasa mtu anayetambulika kuwa ndiye mfupi kuliko wote duniani ni Junrey Balawing toka Filipino ambaye ana urefu wa sentimita 59.93.

Chandra kwa urefu wake wa sentimita 56 anatarajiwa kuivunja rekodi hiyo kirahisi na kutangazwa rasmi kama mtu mfupi kuliko watu wote waliowahi kutokea duniani.

Tuesday, May 10, 2016

JE UNAIJUA  KLABU INAYOIBUA VIPAJI HAPA NCHINI?

Na Yasini Shabani
Mpenzi msomaji wa safu hii ya makala ya michezo na wachezaji leo inajikita kwa kuangalia klabu inayoibua vipaji vya wachezaji chipukizi na wanakuwa msaada mkubwa katika timu ya taifa ya Tanzania.

Kabla hatujaanza kuangalia klabu inayotoa wachezaji wazuri hapa nchini kwanza tuanzie kule kunako ligi kuu ya uingereza ambayo ndio ligi kuu maarufu  duniani ukilinganisha na ligi zingine kama seria A,ya italia,Bundasliga,ya ujerumani,Laliga ya Hispania,League one ya ufaransa na ligi zingine dunianiani.

Klabu nyingi za uingereza zimekuwa zikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kununua wachezaji mazuri ili ziweze kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na ligi kuu nchini humo na michuano ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA CHAMPION LEAGUE).

Licha ya vilabu hivyo kutumia gharama kubwa kwa kufanya usajili lakini Arsenal ndio klabu pekee inayotumia kasi kidogo cha fedha kwa ajili ya usajili kwa kuwa inanunua wachezaji wenye umri mdogo na ambao bado hawajawa mastaa na pindi wanaonekana kuwa wazuri wanawauza kwa bei kubwa.

Na hii imekuwa ikiipa Arsenal faida kubwa kutokana na mauzo ya wachezaji hao na pesa hizo kutumika kwa mambo mbalimbali yanayohusu klabu ikiwa na pamoja na kufanya usajili mzuri.

Hapa nchini Tanzania huwezi ukazungumzia klabu inayozalisha vipaji vya wachezaji bila kuitaja klabu ya soka ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro na inamilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mtibwa.

Klabu hii ambayo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1988 na mwaka 1989 ikashiriki ligi ya wilaya na kucheza ligi kuu mnamo mwaka 1996. Pia klabu hii imewahi kutoa taji la ligi kuu bara mara mbili mfululizo.

Mtibwa sugar kama anavyopenda kusema msemaji wake Tobias Kifaru ni kituo cha kunoa wachezaji wa zamani na wapya msemo huu unajidhihirisha kwamba mtibwa sugar ndio kituo cha kunoa wachezaji wapya na wazamani pale tunapoona inaibua vipaji ambavyo vilikuwa havijulikani.

Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wengi chipukizi wanatoka Mtibwa na wanapoonyesha uwezo wao wamekuwa wakinunuliwa na klabu za Yanga FC,Azam FC na Simba Sc na hatimaye kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa.

Miongoni mwa wachezaji waliowahi kupitia Mtibwa sugar na baadae kujiunga na vilabu vingine ni mlinzi wa kulia wa Yanga Juma Abduli,Ame Aly Zungu wa Azamu,Shabani Kado,Musa Mgosi,Yusufu Macho,Mau Mkami,Said Mkopi,Salum Mayanga,Mecky Mexime,Salum Swedi na  nyota wengine wengi waliowahi kutamba na wakata miwa hao.

Pia Mtibwa ndio klabu pekee hapa nchini yenye uwezo wa kufufua viwango vya wachezaji ambao wanaonekana uwezo wao wa kusakata kabumbu kushuka na kurudi tena wakiwa na kiwango cha hali ya juu kabisa na baadae kuitwa timu ya taifa.

Hao ni baadhi ya wachezaji wa mtibwa sugar wa kijiandaa kucheza mechi
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji ambao walionekana viwango vyao vimeshuka na waliporudi mtibwa wakawa tishio tena kwa wapinzani wao ni Said Bahanuzi akitokea Yanga,Musa Hassani Mgosi akitokea Dc mtema pembe ya DRC,Husseni Javu,Vicent Barnabas  na mlinda mlango Said Mohamedi wote wakitokea Yanga,Issa Rashidi(baba ubaya) na Henry Joseph Shindika wote wakitokea Simba.

Licha ya klabu hii kujikita  kuinua vipaji vya wachezaji chipukizi na wa zamani pia inajali sana kuwa na wachezaji wazalendo na mara nyingi wanawaajiri makocha wazalendo na waliowahi kuchezea mtibwa kuliko walimu wa kigeni.

Pia Mtibwa sugar ni klabu pekee Tanzania ambayo haijawahi kushuka daraja tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1988 ukiziacha klabu mbili yaani Simba na Yanga kwani zipo timu ambazo zilionekana ni tishio kwa soka la hapa nyumbani kwa miaka ya nyuma lakini zilishuka daraja na kupotea kabaisa katika ramani ya mpira wa miguu.
Miongoni mwa klabu hizo ni kama Mji mpwapwa,Kahama united ya shinyanga,CDA ya Dodoma,Tukuyu stars ya mbeya,Kariakoo lindi,Reli ya Morogoro,Pamba ya Mwanza na vilabu vingine ambavyositaweza kuvitaja vyote hivi ni baadhi tu.

Huu uwe ni mfano wa kuigwa na vilabu vikongwe yaani Simba na Yanga wanainua vipaji vya wachezaji wa jitanzania na kuacha kukimbilia kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kununua wachezaji wan je ya nchi na wanakuwa na uwezo sawa na hawa wa ndani ya nchi.


KWA HAYA ALIYOYAONGEA RAIS MAGUFULI YASIPUUZWE

Na yasin shabani
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati anafungua majengo mawili ya mashirika ya mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na PPF mkoani Arusha alizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maslahi ya Taifa ikiwemo kukuza uchumi wa nchi na upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Rais magufuli aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza zaidi katika viwanda ili kutoa nafasi za ajira kwa vijana kuliko kuendelea kujenga majengo makubwa na ya gharama kubwa ambayo hayana msaada  au faida kwa mwananchi wa kawaida.

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh joseph pombe magufuli


Rais alisema kuwa majengo yanayojengwa na mashika hayo mara nyingi yamekuwa hayawanufaishi wananchi wa kawaida na ukizingatia ujenzi wake unatumia mabilioni ya pesa na yanakuwa hayana wapangaji kutokana na bei zao kutokuwa raffiki kwa wananchi walio wengi kwa kuwa vipato vyao ni vidogo na haviwaruhusu kumudu gharama za kupanga kwenye majengo hayo.
Rais hakuishia hapo aliendelea kuzungumza na kuwataka wabadilike na waache kuwekeza katika mambo ambayo hayawasaidii wananchi badala yake waweke nguvu zao katika uwekezaji wa viwanda ili viweze kuwasaidia watanzania pamoja na kukuza uchumi wa taifa na kuacha kuwa tegemezi.

Rais alisema kuwa ni aibu kubwa kwa nchi kama hii ambayo imejaa raslimali nyingi haina viwanda na kukaa kutegemea bidhaa ambazo zitokanazo na vitu vya hapa nchini zinazotengenezwa nje ya nchi hali ya kuwa malighafi yamechukuliwa hapa kwetu.
Pia rais alitoleamfano baadhi ya maeneo kama Tanga ambapo amesema kuna matunda mengi wangeweza kujenga kiwanda cha kusindika matunda na maeneneo ya mikoa ya kanda ya ziwa kuna pamba inalimwa kwa wingi na wangeweza kujenga kiwanda cha nguo na kuwasaidia wakulima kuwa na soko la kuuzia pamba yao kiurahisi kuliko kusubiri kusafisha kwa umbali mrefu au kulanguliwa au kukopwana serikali mwishowe kuishia kudhulumiwa.

Hata hivyo alitolea mfano mwingine ambapo alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye mifugo mingi sana na katika nchi za bara la Afrika inashika nafasi ya pili yakuwa na mifugo mingi ikiongozwa na Ethiopia na Sudan ikiwa ya tatu na kusema kuwa cha kushangaza tanzania hakuna hata kiwanda cha ngozi ambayo ingetumika kutengenezea viatu, mikanda na kadhalika na kusaidia kutoa ajira kwa watanzania na kumnufaisha mfugaji kwa kuuza ngozi ya mnyama wake.

Kutokana na maneno aliyoyaongea Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania tukiangalia kwa undani yana umuhimu mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa nhi yetu na ni jambo jema kwa kuliona hili kwani uchumi wa taifa lolote lile hauwezi kukua bila kuwa na viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa.

Na viwanda hivi vinakuwa na faida nyingi licha ya kutengeneza bidhaa kwa mfano kiwanda cha suukari kinakuwakinawasaidia wananchi kupata sukari ya ndani,kiwanda cha ngozi,kiwanda cha kusindika juisi, pia vinakuwa vinamsaidia mkulima wa miwa kuwa na uhakika wa kupata soko,mfugaji kuuza ngozi na kufurahia kazi yake ya ufugaji na pia kinatoa fursa za ajira kwa vijana ambao wanazagaa mitaani kwa kukosa kazi


Haya maneno aliyoyasema rais yana umuhimu na si ya kuyachukulia kiuepesi kuwa hii mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na mashirika mengine watumie elimu zao kama rais alivyosema ili wabadilishe mwelekeo na kuacha kuwekeza katika mambo ambayo hayawanufaishi wananchi ni kama anasa na badala yake wajenge viwanda na kuwaajiri watanzania na kupunguza wimbi la ukosefu ajira nchini. 

Thursday, May 5, 2016

NANI KAMA JUMA ABDULI JAFFARI
Na Yasini Shabani
Unapozungumzia mabeki wanaotisha kwa kipindi hiki hapa nchini Tanzania huwezi kumuacha mlinzi wa kulia wa Mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Dar es salaam Yanga Africans  simwingi bali ni Juma Abduli Jaffari

Mlinzi huyu wa kitanzania alijiunga na Klabu ya Dar es salaam Yanga Africans akitokea klabu ya Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani morogoro ni mara baada ya kuonyesha uwezo wake wa kucheza soka na dipo kupelekea uongozi wa wanajangwani hao kuamua kumpa mkataba wa kuitumikia Yanga kwa mashindano mbalibali.
Juma Abduli akiwa anapata maelekezo toka kwa kocha wake

Juma Abduli alipofika jangwani alikumbana na upinzani mkali wa kuwania namba katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa kihistoria hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla wakipambana vikali na  Mwanda Mbuyu Twitte ambaye alikuwa katika kiwango cha juu kabisa na kila mmoja akitaka kumuweka mwenzake benchi.

Licha ya kupata upinzani huo kutoka kwa Mbuyu Twitte Abduli pia alikumbana na majeruhi ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu na kumpelekea kuhatarisha kuua kiwango chake na kurudi katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao.

Baada ya kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu  Abduli alipopona majeraha yake alirudi uwanjani akiwa katika kiwango bora na kumpa wakati mgumu kocha wake kushindwa kujua nani amnzishe na nani akae benchi kutokana na walinzi hao wote kuonekana wanauwezo wa kuimudu nafasi hiyo ya pembeni.

Kadri muda unavyozidi kwenda Juma Abduli alifanikiwa kumnyang’anya namba Mbuyu Twitte ambaye anaonekana kuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani pamoja na kusifika kwa kurusha mipira mirefu inayofananishwa na kona.

Kwa kipindi hiki Mlinzi huyu amekuwamsaada mkubwa sana kwa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara na kuiwezesha timu yake kushika usikani na katika michezo ya kimataifa na kuifikisha kufika fainali ya kombe la shirikisho linaloandaliwa na Azamu.
Licha ya kucheza eneo la mlinzi wa pembeni kulia(Right fullback) upande wa kulia pia ana uwezo mkubwa wa kunzisha mashambulizi akitokea nyuma na kupiga mpira ya krosi na kukutana na washambuliaji Amisi Tambwe na Donald Ngoma ambao wamekuwa wanaitumia vizuri kwa kufunga magoli.

Pia ameweza kuibeba Yanga katika michezo mbalimbali ukiwemo dhidi ya  Azam ambapo alifunga goli la kusawazisha kwa shoti kali na mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2,dhidi ya APR ya Rwanda mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika alifunga kwa mkwaju mkali wa adhabu ndogo na kuipa timu yake bao la kuongoza na baadae Ngoma kufunga la pili kabla ya wenyeji kupata goli la kufutia machozi.

Mchezo mwingine ni wa klabu bingwa Afrika dhidi ya waarabu wa Al ahal ya misri ni pale alipotoa basi murua ambayo ilimkuta Donald Ngoma na kuuweka mpira nyavuni na ni goli la kusawazisha kwa upande wa Yanga lakini mcherzo huo ulimalizika kwa Yanga kupoteza  kwa  mabao 2-1.na waarabu hao wenye historia kubwa barani Afrika.

Hii ni moja ya somo kwa wachezaji wa kitanzania wanaochipukia kuiga mfano wa Juma Abduli kwa kutokata tamaa kwani tumekuwa tukishuhudia wachezaji wengi wakiibuka na kupotea kwenye ulimwengu wa soka .Vijana wetu wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kwa kukata tama kitendo ambacho ni hatari kwa maisha ya mchezaji mwenye umri mdogo.

KWA HISTORIA ZAIDI YA JUMA ABDULI KUHUSU MAISHA YAKE YA MPIRA WA MIGUU USIKOSE MAKALA IJAYO HAPA 

Wednesday, May 4, 2016

Atletico Madrid yatinga fainali ligi ya mabingwa

  • 4 Mei 2016
na bbc
GriezmannImage copyrightReuters
Image captionGriezmann alifungia Atletico bao la kusawazisha
Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Atletico wakiwa na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza nchini Uhispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Xabi Alonso kwenye mechi ya Jumanne iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya mshambuliaji Antoine Griezmann kusawazisha na kuwa 1-1.
MadridImage copyrightEPA
Image captionAtletico Madrid wamefuzu kwa fainali itakayochezwa 28 Mei
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres kuokolewa na mlinda mlango Manuel Neuer.
Matokeo ya jumla ya nusufainali hiyo yalimalizika sare 2-2 lakini Madrid wakasonga kwa kuwa na bao la ugenini.
Sasa Atletico watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu katika fainali mjini Milan tarehe 28 Mei.

Tuesday, May 3, 2016

YANGA AFRICAN'S LEO 3 MAY 2016 INAYO TALAJIA KUCHEZA  NA WANA WASHINYANGA STAND UNITED,YANGA IKIWA UGENINI
chanzo na habari leo
VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga leo watakuwa wenyeji wa Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo wakitokea Jijini Mwanza, ambapo Jumamosi iliyopita iliifunga Toto Africans na kujiimarisha kileleni kwa kufikisha pointi 65, wakati wenyeji wao Stand siku hiyo walikubali kipigo cha mabao 2-1, kutoka kwa Mwadui FC, mchezo uliopigwa Uwanja wa Mwadui Complex.
Yanga tayari wametua mkoani Shinyanga tangu Jumapili kujiandaa na mchezo huo huku wakiwa wamepania kupata pointi tatu ambazo zitazidi kuwaweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao msimu huu ambao unashirikisha timu 16.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani Stand United inayoshika nafasi ya saba kwenye msimamo na pointi zao 34, hawatakubali kupoteza mchezo mwingine tena wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Kocha wa Stand United, Mfaransa Patrick Liewig, alisema amekiandaa vizuri kikosi chake kwa ajili ya kushinda mchezo huo ambao utawasaidia kumaliza msimu kwenye nafasi nzuri zaidi kuliko waliyo sasa.
Liewig alisema anajua anakwenda kupambana na timu ngumu inayoongoza ligi lakini wamejipanga kuhakikisha wanacheza vizuri na kushinda kutokana na maandalizi waliyoyafanya mara baada ya kumalizika mchezo wao uliopita dhidi ya Mwadui FC.
Katika mchezo huo, kocha Liewig atakuwa akiwategemea zaidi wachezaji wake Elias Maguli, kiungo Amri Kiemba na Haruna Changongo ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chake huku safu ya ulinzi ikiwa chini ya Nassor Masoud ‘Chollo’ , Abuu Ubwa na Rajabu Zahiri.
Kwa upande wake kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, alisema amekwenda Shinyanga kwa ajili ya pointi tatu na ana uhakika wa kuzipata kutokana na uimara wa kikosi chake ambacho kimekuwa kikiimarika katika kila mechi wanayocheza hivi sasa.
Pluijm alisema anaiheshimu Stand United kuwa ni moja ya timu nzuri na ngumu ambayo inaundwa na wachezaji wengi wazoefu, lakini anajivunia ubora wa wachezaji wake ambao ushiriki wao katika michuano ya kimataifa umewapa uzofu mkubwa na ndiyo sababu ya matokeo ya ushindi wanao upata.
Pluijm alisema kikosi chake cha leo hakitakuwa na mabadiliko makubwa sana tofauti na kile kilichoanza kwenye mchezo ulipita dhidi ya Toto Africans, ambapo katika safu ya ushambuliaji akiendelea kuwatumia mapacha wawili Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao wote kwa pamoja wamefunga mabao 33.