JE UNAIJUA KLABU
INAYOIBUA VIPAJI HAPA NCHINI?
Na Yasini Shabani
Mpenzi msomaji wa safu hii ya makala ya michezo na wachezaji
leo inajikita kwa kuangalia klabu inayoibua vipaji vya wachezaji chipukizi na
wanakuwa msaada mkubwa katika timu ya taifa ya Tanzania.
Kabla hatujaanza kuangalia klabu inayotoa wachezaji wazuri
hapa nchini kwanza tuanzie kule kunako ligi kuu ya uingereza ambayo ndio ligi
kuu maarufu duniani ukilinganisha na
ligi zingine kama seria A,ya italia,Bundasliga,ya ujerumani,Laliga ya Hispania,League
one ya ufaransa na ligi zingine dunianiani.
Klabu nyingi za uingereza zimekuwa zikitumia kiasi kikubwa
cha fedha kwa ajili ya kununua wachezaji mazuri ili ziweze kufanya vizuri
katika mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na ligi kuu nchini humo na
michuano ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA CHAMPION LEAGUE).
Licha ya vilabu hivyo kutumia gharama kubwa kwa kufanya
usajili lakini Arsenal ndio klabu pekee inayotumia kasi kidogo cha fedha kwa
ajili ya usajili kwa kuwa inanunua wachezaji wenye umri mdogo na ambao bado
hawajawa mastaa na pindi wanaonekana kuwa wazuri wanawauza kwa bei kubwa.
Na hii imekuwa ikiipa Arsenal faida kubwa kutokana na mauzo
ya wachezaji hao na pesa hizo kutumika kwa mambo mbalimbali yanayohusu klabu
ikiwa na pamoja na kufanya usajili mzuri.
Hapa nchini Tanzania huwezi ukazungumzia klabu inayozalisha
vipaji vya wachezaji bila kuitaja klabu ya soka ya Mtibwa Sugar ya mkoani
Morogoro na inamilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mtibwa.
Klabu hii ambayo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1988 na
mwaka 1989 ikashiriki ligi ya wilaya na kucheza ligi kuu mnamo mwaka 1996. Pia
klabu hii imewahi kutoa taji la ligi kuu bara mara mbili mfululizo.
Mtibwa sugar kama anavyopenda kusema msemaji wake Tobias
Kifaru ni kituo cha kunoa wachezaji wa zamani na wapya msemo huu
unajidhihirisha kwamba mtibwa sugar ndio kituo cha kunoa wachezaji wapya na
wazamani pale tunapoona inaibua vipaji ambavyo vilikuwa havijulikani.
Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wengi chipukizi wanatoka
Mtibwa na wanapoonyesha uwezo wao wamekuwa wakinunuliwa na klabu za Yanga
FC,Azam FC na Simba Sc na hatimaye kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa.
Miongoni mwa wachezaji waliowahi kupitia Mtibwa sugar na
baadae kujiunga na vilabu vingine ni mlinzi wa kulia wa Yanga Juma Abduli,Ame
Aly Zungu wa Azamu,Shabani Kado,Musa Mgosi,Yusufu Macho,Mau Mkami,Said
Mkopi,Salum Mayanga,Mecky Mexime,Salum Swedi na nyota wengine wengi waliowahi kutamba na
wakata miwa hao.
Pia Mtibwa ndio klabu pekee hapa nchini yenye uwezo wa
kufufua viwango vya wachezaji ambao wanaonekana uwezo wao wa kusakata kabumbu
kushuka na kurudi tena wakiwa na kiwango cha hali ya juu kabisa na baadae
kuitwa timu ya taifa.
Hao ni baadhi ya wachezaji wa mtibwa sugar wa kijiandaa kucheza mechi
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji ambao walionekana viwango
vyao vimeshuka na waliporudi mtibwa wakawa tishio tena kwa wapinzani wao ni
Said Bahanuzi akitokea Yanga,Musa Hassani Mgosi akitokea Dc mtema pembe ya DRC,Husseni
Javu,Vicent Barnabas na mlinda mlango
Said Mohamedi wote wakitokea Yanga,Issa Rashidi(baba ubaya) na Henry Joseph
Shindika wote wakitokea Simba.
Licha ya klabu hii kujikita kuinua vipaji vya wachezaji chipukizi na wa
zamani pia inajali sana kuwa na wachezaji wazalendo na mara nyingi wanawaajiri
makocha wazalendo na waliowahi kuchezea mtibwa kuliko walimu wa kigeni.
Pia Mtibwa sugar ni klabu pekee Tanzania ambayo haijawahi
kushuka daraja tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1988 ukiziacha klabu mbili
yaani Simba na Yanga kwani zipo timu ambazo zilionekana ni tishio kwa soka la
hapa nyumbani kwa miaka ya nyuma lakini zilishuka daraja na kupotea kabaisa
katika ramani ya mpira wa miguu.
Miongoni mwa klabu hizo ni kama Mji mpwapwa,Kahama united ya
shinyanga,CDA ya Dodoma,Tukuyu stars ya mbeya,Kariakoo lindi,Reli ya
Morogoro,Pamba ya Mwanza na vilabu vingine ambavyositaweza kuvitaja vyote hivi
ni baadhi tu.
Huu uwe ni mfano wa kuigwa na vilabu vikongwe yaani Simba na
Yanga wanainua vipaji vya wachezaji wa jitanzania na kuacha kukimbilia kutumia
gharama kubwa kwa ajili ya kununua wachezaji wan je ya nchi na wanakuwa na
uwezo sawa na hawa wa ndani ya nchi.
No comments:
Post a Comment