KWA HAYA ALIYOYAONGEA
RAIS MAGUFULI YASIPUUZWE
Na yasin shabani
Rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania wakati anafungua majengo mawili ya mashirika ya mifuko
ya hifadhi ya jamii NSSF na PPF mkoani Arusha alizungumzia mambo mbalimbali
yanayohusu maslahi ya Taifa ikiwemo kukuza uchumi wa nchi na upatikanaji wa
ajira kwa vijana.
Rais magufuli
aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza zaidi katika viwanda ili kutoa
nafasi za ajira kwa vijana kuliko kuendelea kujenga majengo makubwa na ya
gharama kubwa ambayo hayana msaada au
faida kwa mwananchi wa kawaida.
Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh joseph pombe magufuli
Rais alisema kuwa
majengo yanayojengwa na mashika hayo mara nyingi yamekuwa hayawanufaishi
wananchi wa kawaida na ukizingatia ujenzi wake unatumia mabilioni ya pesa na
yanakuwa hayana wapangaji kutokana na bei zao kutokuwa raffiki kwa wananchi
walio wengi kwa kuwa vipato vyao ni vidogo na haviwaruhusu kumudu gharama za
kupanga kwenye majengo hayo.
Rais hakuishia
hapo aliendelea kuzungumza na kuwataka wabadilike na waache kuwekeza katika
mambo ambayo hayawasaidii wananchi badala yake waweke nguvu zao katika
uwekezaji wa viwanda ili viweze kuwasaidia watanzania pamoja na kukuza uchumi
wa taifa na kuacha kuwa tegemezi.
Rais alisema kuwa
ni aibu kubwa kwa nchi kama hii ambayo imejaa raslimali nyingi haina viwanda na
kukaa kutegemea bidhaa ambazo zitokanazo na vitu vya hapa nchini zinazotengenezwa
nje ya nchi hali ya kuwa malighafi yamechukuliwa hapa kwetu.
Pia rais
alitoleamfano baadhi ya maeneo kama Tanga ambapo amesema kuna matunda mengi wangeweza
kujenga kiwanda cha kusindika matunda na maeneneo ya mikoa ya kanda ya ziwa
kuna pamba inalimwa kwa wingi na wangeweza kujenga kiwanda cha nguo na
kuwasaidia wakulima kuwa na soko la kuuzia pamba yao kiurahisi kuliko kusubiri
kusafisha kwa umbali mrefu au kulanguliwa au kukopwana serikali mwishowe
kuishia kudhulumiwa.
Hata hivyo
alitolea mfano mwingine ambapo alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye mifugo mingi
sana na katika nchi za bara la Afrika inashika nafasi ya pili yakuwa na mifugo
mingi ikiongozwa na Ethiopia na Sudan ikiwa ya tatu na kusema kuwa cha
kushangaza tanzania hakuna hata kiwanda cha ngozi ambayo ingetumika
kutengenezea viatu, mikanda na kadhalika na kusaidia kutoa ajira kwa watanzania
na kumnufaisha mfugaji kwa kuuza ngozi ya mnyama wake.
Kutokana na
maneno aliyoyaongea Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania tukiangalia
kwa undani yana umuhimu mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa nhi yetu na ni
jambo jema kwa kuliona hili kwani uchumi wa taifa lolote lile hauwezi kukua
bila kuwa na viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa.
Na viwanda hivi vinakuwa
na faida nyingi licha ya kutengeneza bidhaa kwa mfano kiwanda cha suukari kinakuwakinawasaidia wananchi kupata sukari ya ndani,kiwanda
cha ngozi,kiwanda cha kusindika juisi, pia vinakuwa vinamsaidia mkulima wa miwa
kuwa na uhakika wa kupata soko,mfugaji kuuza ngozi na kufurahia kazi yake ya
ufugaji na pia kinatoa fursa za ajira kwa vijana ambao wanazagaa mitaani kwa
kukosa kazi
Haya maneno
aliyoyasema rais yana umuhimu na si ya kuyachukulia kiuepesi kuwa hii mifuko ya
hifadhi ya jamii pamoja na mashirika mengine watumie elimu zao kama rais
alivyosema ili wabadilishe mwelekeo na kuacha kuwekeza katika mambo ambayo
hayawanufaishi wananchi ni kama anasa na badala yake wajenge viwanda na
kuwaajiri watanzania na kupunguza wimbi la ukosefu ajira nchini.
No comments:
Post a Comment