NANI KAMA JUMA ABDULI JAFFARI
Na
Yasini Shabani
Unapozungumzia mabeki wanaotisha kwa kipindi hiki
hapa nchini Tanzania huwezi kumuacha mlinzi wa kulia wa Mabingwa watetezi na
vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Dar es salaam Yanga Africans simwingi bali ni Juma Abduli Jaffari
Mlinzi huyu wa kitanzania alijiunga na Klabu ya Dar
es salaam Yanga Africans akitokea klabu ya Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani
morogoro ni mara baada ya kuonyesha uwezo wake wa kucheza soka na dipo
kupelekea uongozi wa wanajangwani hao kuamua kumpa mkataba wa kuitumikia Yanga
kwa mashindano mbalibali.
Juma Abduli alipofika jangwani alikumbana na upinzani
mkali wa kuwania namba katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa kihistoria
hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla wakipambana vikali na Mwanda Mbuyu Twitte ambaye alikuwa katika
kiwango cha juu kabisa na kila mmoja akitaka kumuweka mwenzake benchi.
Licha ya kupata upinzani huo kutoka kwa Mbuyu Twitte
Abduli pia alikumbana na majeruhi ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa muda
mrefu na kumpelekea kuhatarisha kuua kiwango chake na kurudi katika kikosi cha
kwanza cha mabingwa hao.
Baada ya kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu Abduli alipopona majeraha yake alirudi
uwanjani akiwa katika kiwango bora na kumpa wakati mgumu kocha wake kushindwa
kujua nani amnzishe na nani akae benchi kutokana na walinzi hao wote kuonekana
wanauwezo wa kuimudu nafasi hiyo ya pembeni.
Kadri muda unavyozidi kwenda Juma Abduli alifanikiwa
kumnyang’anya namba Mbuyu Twitte ambaye anaonekana kuwa na uwezo wa kucheza
nafasi nyingi uwanjani pamoja na kusifika kwa kurusha mipira mirefu
inayofananishwa na kona.
Kwa kipindi hiki Mlinzi huyu amekuwamsaada mkubwa
sana kwa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara na kuiwezesha timu yake
kushika usikani na katika michezo ya kimataifa na kuifikisha kufika fainali ya
kombe la shirikisho linaloandaliwa na Azamu.
Licha ya kucheza eneo la mlinzi wa pembeni kulia(Right
fullback) upande wa kulia pia ana uwezo mkubwa wa kunzisha mashambulizi
akitokea nyuma na kupiga mpira ya krosi na kukutana na washambuliaji Amisi
Tambwe na Donald Ngoma ambao wamekuwa wanaitumia vizuri kwa kufunga magoli.
Pia ameweza kuibeba Yanga katika michezo mbalimbali
ukiwemo dhidi ya Azam ambapo alifunga
goli la kusawazisha kwa shoti kali na mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2,dhidi
ya APR ya Rwanda mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika alifunga kwa mkwaju
mkali wa adhabu ndogo na kuipa timu yake bao la kuongoza na baadae Ngoma kufunga
la pili kabla ya wenyeji kupata goli la kufutia machozi.
Mchezo mwingine ni wa klabu bingwa Afrika dhidi ya
waarabu wa Al ahal ya misri ni pale alipotoa basi murua ambayo ilimkuta Donald
Ngoma na kuuweka mpira nyavuni na ni goli la kusawazisha kwa upande wa Yanga
lakini mcherzo huo ulimalizika kwa Yanga kupoteza kwa mabao 2-1.na waarabu hao wenye historia kubwa
barani Afrika.
Hii ni moja ya somo kwa wachezaji wa kitanzania
wanaochipukia kuiga mfano wa Juma Abduli kwa kutokata tamaa kwani tumekuwa
tukishuhudia wachezaji wengi wakiibuka na kupotea kwenye ulimwengu wa soka
.Vijana wetu wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kwa kukata tama kitendo
ambacho ni hatari kwa maisha ya mchezaji mwenye umri mdogo.
KWA
HISTORIA ZAIDI YA JUMA ABDULI KUHUSU MAISHA YAKE YA MPIRA WA MIGUU USIKOSE
MAKALA IJAYO HAPA
No comments:
Post a Comment