Ukisikia mtu mfupi kuliko wote duniani basi huyu mwanaume wa nchini Nepal atakuwa amevunja rekodi ya dunia, ana urefu wa sentimeta 56 na uzito wa kilo 12 tu.
Chandra Bahadur Dangi akiwa amesimama wima kuonyesha urefu wake wa sentimita 56 tu | ||
Maafisa wa kitabu cha rekodi za dunia, Guinness World Records wanatarajiwa kusafiri kwenda nchini Nepal kukutana na mtu mfupi kuliko watu wote wafupi waliowahi kuishi duniani. Babu mwenye umri wa miaka 72, Chandra Bahadur Dangi ana urefu wa sentimita 56 na uzito wa kilo 12 tu na anaishi kwenye kijiji kilichopo kwenye mabonde yaliyopo kusini magharibi mwa Nepal. Kwa miaka mingi babu Chabdra amekuwa akiishi kwenye kijiji hicho akijipatia umaarufu kwa ufupi wake hadi hivi karibuni televisheni ya taifa ya Nepal ilipomuonyesha na kumpima urefu kucheki kama amevunja rekodi ya dunia. Kugundulika kwa Chandra kuwa ni mfupi kuliko watu wote duniani kumemfanya Chandra ajipatie umaarufu wa ghafla nchini Nepal na duniani. "Tunaenda Nepal kwenye kijiji cha Chandra ili kuthibitisha urefu wake na kumtangaza rasmi kuwa mtu mfupi kuliko wote duniani", alisema afisa wa Guiness worldrecords, Craig Glenday. Ndugu wa Chandra walisema kuwa Chandra ana afya njema hajawahi kuugua wala kwenda hospitali na hatumii dawa zozote. Kwa hivi sasa mtu anayetambulika kuwa ndiye mfupi kuliko wote duniani ni Junrey Balawing toka Filipino ambaye ana urefu wa sentimita 59.93. Chandra kwa urefu wake wa sentimita 56 anatarajiwa kuivunja rekodi hiyo kirahisi na kutangazwa rasmi kama mtu mfupi kuliko watu wote waliowahi kutokea duniani. |
No comments:
Post a Comment