Na Edger Alexander
Ifahamu Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu.
Mahakama hii ambayo makao makuu yake yako Arusha nchini
Tanzania ni mahakama ya bara zima la
Afrika ambapo ilianzishwa na nchi wanachama wa umoja wa Afrika (AU) ili
kumimarisha haki za binadamu na watu Barani Afrika na ilianzishwa kwa mujibu wa
kifungu namba 1 cha itifaki ya mkataba wa Afrika wa Haki za binadamu na watu ya
kuanzishwa kwa Mhakama ya Afrika ya Haki za Binadamau na watu.
Itifaki hiyo hiyo ilikubaliwa Juni 9 mwaka 1998 nchini
Bukinafaso na ikaanza kutumika Januari 25 mwaka 2004 na Mahakama ilianza
Shughuli zake rasmi mwezi Novemba mwaka 2006 ambapo kazi yake kuu ilikuwa ni
kukamilisha na kuimarisha jukumu la kulinda haki za Tume ya Afrika ya Haki za
Binadamu na watu(Maarufu kama Tume ya Banju).
Tangu kukubaliwa kwa itifaki hiyo mwaka 1998,ni nchi 29 tu
kati ya nchi 54 wanachama wa umoja wa Afrika ndizo zilizoridhia itifaki hiyo
ambapo nchi hizo ni pamoja na
AfrikaKusini,Algeria,Benin,Burkinafaso,Burundi,Cameroon,Comoros,Gabon
Gambia,Ghana,Ivory Coast,Jamuhuri ya Kidemokrasia yaKongo,Kenya,Libya,Lesotho,Malawi,Mali,Mauritania,Mauritrius,Msumbiji,Nigeria,Niger,Uganda,Rwanda,Senegal,Togo,Tunisia
pamoja na Tanzania.
Ujumbe wa Mahakama hii ni kuhimarisha jukumu la kulinda haki
za Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa kuongeza usimamizi imara wa
mfumo wa Haki za Binadamu Afrika na kuhakikisha,kuheshimika na kuridhiwa kwa
mujibu wa mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu pia mikataba mingine ya
Kimataifa ya Haki za Binadamu kupitia maamuzi ya Mahakama.
Pamoja na hatua ya kuridhiwa kwa itifaki,nchi wanachama
zinatakiwa kutoa tamko kwa mujibu wa kifungu cha 34(6) cha itifaki ya kukubali
kuruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuleta kesi moja
kwa moja mbele ya Mahakama hii, bila kutolewa kwa tamko la namana hiyo Mahakama
haitakuwa na malaka ya kushughulikia kesi zinazotolewa mbele yake na watu
binafsi na Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs)
Hadi kufikia Januari 2015,ni nchi 7 tu kati ya 29
zilizoridhia itifaki ndizo zilitoa tamko la kukubali mamlaka ya Mahakama kuweza
kupokea kesi za watu binafsi na NGOs,nchi hizo ni pamoja na Bukinafaso,Ivory
Coast,Ghana,Malawi,Mali,Rwanda na Tanzania.
Mahakama hii ina majaji kumi na moja (11) ambao ni raia wa
nchi wanachama wa umoja wa Afika (AU).Majaji hao huchaguliwa na wakuu wa nchi
na Serikli za Umoja wa Afrika kwa muda wa miaka sita (6) na wanaweza
kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kimoja (yaani mika 6 mingine),pia majaji
hao huchaguliwa baada ya kuteuliwa na nchi zao kutokana na nafasi zao,uadilifu
wao pamoja na ueledi wa kazi
unaotambulika kimahakama au kimasomo katika nyanja ya Haki za Binadamu za watu.
Nchi zote wanachama wa umoja wa Afrika ambazo zimeridhia
itifaki ya kuanzishwa kwa Mahakama zinaweza kuteua wagombea wa nafasi ya Jaji wa
Mahakama na idai ya majaji inagawanya kwa mujibu wa kanda mbali mbali za
Afrika.Majaji wa Mahakama hiyo kwa sasa
ni jaji Augustino Ramadhani ambaye ni
Rais wa Mahakama hiyo akitokea Tanzania na makamu wake ni Jaji Elsie Thompson
ambaye anatokea katika nchi ya Nigeria.
Wengine ni Jaji Gerard Niyungeko(Burundi) Jaji Fatsah
Ouguergous(Algeria),Jaji Duncan Tambala (Malawi),Jaji Sylvain Ore (Ivory
Coast),Jaji El Hadj Guisse (Senegal) Jaji Ben Kioko (Kenya),Jaji Rafaa Achor
(Tunisia),Jaji Solomy Bossa (Uganda) na Jaji Angelo Matusse (Msumbiji).
Toka ianze kazi zake rasmi mwezi Novemba,mwaka 2006 AddisAbaba nchini Ethiopia,kabla ya mwezi
Agosti,mwaka 2007 kuhamishia makao makuu
yake Arusha nchini Tanzania ambako Serikali imeipatia Makahama hiyo ofisi ya
muda ikisubili ujenzi wa ofisi yake ya kudumu ambapo imeweza kupata mafaniko
makubwa ambayo yameifanya izidi kuimarika katika kutekelza majukumu yake kwa
bara zima la Afrika.
Mahakama hii yenye mamlaka mawili ambayo ni kuamua kesi na
kutoa ushauri,hadi mwezi Januari mwaka 2015 ilikwishapokea kesi 32 na kesi 20
kati ya hizo zimekwisha shughulikiwa na zipo kesi 8 ambazo bado zinashughulikwa
pamoja na maombi manne (4) ya kutaka ushauri wa kisheria ambapo hatua hiyo
inatajwa kuwa ni moja ya mafaniko makubwa ndani ya Mahakama hiyo.
Mahakama hii ilitoa hukumu yake ya kwanza mwaka 2009
kufuatia ombi la lililowasilishwa mbele yake Agosti 11 mwaka 2008 na
mlalamikaji Michelot Yogombaye dhidi Jamuhuri ya Senegal ambapo mlalamikaji aliiomba
Mahakama kusitisha mwenendo wa kesi iliyowasilishwa na Serikali ya Senegal
dhidi ya Hissen Habre Rais wa zamani wa Jamhuri ya Chad anayeishi nchini
Senegal kama mkimbizi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 34 (6) cha itifaki na kanuni ya 33
(f) ya kanuni za Mahakama,Maahakama ilibaini kwamba ombi haliwezi kupokeklewa
kwa sababu Mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa vile Senegal
ilikuwa haijatoa tamko la kuridhia mamlaka ya Mahakama kupokea maombi
yanayowasilishwa moja kwa moja na mtu binafsi au taasisi ya Serikali.
No comments:
Post a Comment