Mipango madhubuti na mbinu mpya.
Katika kuhakikisha Jiji la Arusha linarudisha hadhi yake
kimechezo hasa hasa katika upande wa Soka, uongozi wa jiji hilo umekuja na
mipango madhubuti na mbinu mpaya ikiwa
pamoja na kutenga bajeti maalumu ya kuboresha viwanja vyote vya michezo katika
shule zote za Sekondari na Msingi .
Licha ya kuwa na umaarufu
wa sifa nyingi ikiwemo uzalishaji wa madini mbali mbali pamoja na kuwa
na vivutio vingi vya utalii lakini jiji la Arusha katika upande wa michezo
limedodora sana mpaka kufikia hatua ya kukosa hata timu moja inayoshiriki ligi
kuu Tanzania bara jambo linalowanyima wapenzi wa soka jijini hapa uondo wa
kushuhudia mechi mbali mbali za ligi kuu.
Kukosa hata timu moja
inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara ni aibu kubwa kwa jiji kama
Arusha tena lenye historia ya mambo mbali mbali ikiwemo kuwa eneo lilitoa
Azimio la Arusha na ikumbukwe kuwa endapo soka linatumiwa vizuri inaweza kuwa
kama sehemu mojawapo ya kuliingizia mapato jiji hilo.
Kutokana na hali hiyo uongozi mpya wa Halimashauri ya jiji
la Arusha chini ya meya wake Kalisti Lzaro umeamua kuja na mbinu mpya za kuinua
soka ikiwa pamoja na kutenga bajeti maalumu ya kujenga na kuendeleza viwanja
vya michezo katika shule zote za msingi na Sekondari zenye viwanja ambavyo
mazingira yake hayafai kufanyika michezo ya aina mbali mbali.
Kipindi cha nyuma Timu ya AFC y Arusha iliweza kupeprerusha vyema
bendera ya jiji hilo kisoka ikiwa pamoja na kushika nafasi za juu katika
msimamo wa liguu Tanzania bara lakini
mwishowe ilishuka hadi ligi daraja kwanza na mwaka 2012 timu hiyo ilishuswa
daraja hadi ligi ngazi ya Taifa baada ya
kushindwa kutokea katika mchezo wa Kundi c wa ligi daraja la kwanza dhidi ya
timu ya 94 KJ uliotakiwa kufanyika katika uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi
mkoani Pwani mnamo Februari 15 mwaka 2012.
Timu hiyo kwa sasa inashiriki michezo ya ligi daraja la pili
na bado haijaonesha matumaini ya kupanada ligi daraja la kwanza na hatimaye
kucheza michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Ukiachana na timu ya AFC ya Arusha timu nyingine iliyoweza
kuliwakilisha vyema jiji la Arusha ni timu ya JKT Oljoro ambayo ilionesha
ushindani mkubwa katika michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara na ni moja ya timu zilizotabiliwa makubwa kutokana na soka lililokuwa likoneshwa na
timu hiyo.
Katika kuonesha kuwa jiji la Arusha halina bahati katika
upande wa soka timu hiyo nayo katika msimu
wa mwaka 2013/2014 ilishuka daraja hadi ligi daraja la kwanza na kwa sasa
inakabiliwa na tuhuma za upanagaji wa matokeo katika michezo yake ya ligi
daraja kwanza msimu huu hivyo matarajio ya kuona katika jiji la Arusha
kunachezwa michezo ya ligii kuu soka Tanzania bara kwa msimu ujao yameshapotea
kabisa
.
wa chezaji wa jkt oljoro
Akiongelea sula hilo la katika mkutano wake na waandishi wa
habari hivi karibuni Meya wa jiji hilo Kalist Lazaro alisema kwa sasa
wamejipanga kuinua soka ikiwa pamoja na kuunda timu imara ya mpira wa miguu
ambayo itakuwa bora kwa ajili kuliwakilisha jiji la Arusha katika mashindano
mbali mbali ikiwemo ligi kuu soka Tanzania bara .
“Nawaomba wadau na wapenzi wa soka jijini hapa watoe
ushirikiano wa hali na mali kwa timu itakayopatikana ili kuhakikisha jiji la
Arusha linasonga mbele kimichezo hususani katika soka na kurudisha heshima ya
awali”,alisema Meya Lazaro.
Naye Mwenyekiti wa
Kamati ya huduma za jamii wa Halimsahauri ya jiji la Arusha Isaya Doita Harry akiongea na Fukuto kwa njia ya simu
katika mahojiano maalumu alisema ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa jiji la
Arusha limeshuka katika upande wa michezo lakini akadai kuwa baada ya kuona
hali hayo wameamua kuja na mikakati mizito ya kuinua soka jijini humo.
“Nikiri kabisa kuwa katika upande wa michezo hatujakupa
nafasi ya kutosha ila kwa sasa katika bajeti yetu tuliyopitisha ya mwaka wa
fedha 2016/2017 tushakubaliana kutenga
bajeti ya kutosha na tumekubaliana kuwa
katika shule zote zenye viwanja vya michezo lazima viboreshwe na kuwa katika
ubora unaotakiwa ili kuwapa wanafunzi uwezo wa
kucheza na kuonesha vipaji vyao na hii itatusaidia sana katika kuanza
kuisuka upya michezo katika jiji letu”,alisema Doita.
Aidha alisema jambo lingine linalofanya michezo katika jiji
la Arusha kushuka hususani soka ni kutokana na kuwepo kwa udhaifu mkubwa kwa
viongozi wenye nyazifa katika upande wa michezo ikiwa pamoja na kutokuwa makini
lakini akadai kuwa tayari washaliona jambo hilo hivyo wameamua kulifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment