Serikali yatakiwa kuweka mazingira rafiki kwa wajasiliamali.
Serikali imetakiwa kuweka mazingira rafiki kwa wananchi wote wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo maarufu kama ujasiriamali ili kuwafanya na wao kuwa na wigo mpana wa kuweza kukabiliana na hali ya maisha pamoja na kuchangia katika shughuli za kimaendeleo.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na baadhi ya wanawake ambao wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo ya kulima na kuuza mboga za majani maarufu kama ujasiliamali jijini Arusha katika mahojiano na Fukuto.
Walisema licha ya kuwajengea mazingia mazuri ya kufanya biasahara lakini wanatakiwa kuangaliwa hata upande wa kupewa mikopo ambayo itawawezesha kupanua biashara zao.
"Tunaiomba Serikali kuhakikisha inatuwekea mazingira rafiki watu tunaojishughulisha na biashara hizi ndogo ndogo pamoja na shughuli zote za ujasiriamali kwani inatusaidia katika kuondokana na wimbi la umasikini na pia tutakuwa na wasaa wa kutoa michango katika shughuli za kimaendeleo",alisema moja ya mwanamke mjasiriamali aliyejitambulisha kwa jina moja la Mama Rehema.
Alisema wakiwekewa mazingira rafiki wataweza kujiajiri wenyewe na kuondoa zana ya kusubiri kuajiriwa na mtu au kuajiriwa na Serikali huku akiwataka wanawake wote kuwaiga wao kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali ili kuziendeleza familia zao na kutokuwa tegemezi.
Alisema kwa sasa imepita miaka 10 toka aanze kufanya biasahara hiyo huku akidai kupitia kazi yake hiyo anasomesha watoto wawili mmoja akiwa katika Shule ya sekondari na mwingine akiwa shule ya msingi.
"Mboga zinatumia muda mfupi sana kukua hivyo naweza kupata mahitaji ya familia yangu ikiwa pamoja na kuwasomesha watoto wangu ambapo mmoja yuko ngazi ya Sekondari na mwingine akiwa katika nagazi ya Shule ya msingi",alisema mama Rehema.
Kwa upande wa mama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la mama Hassani alisema mradi huo umemsadia kuwasomesha wanae wawili katika shule za watu binafsi jambo linalomfanaya ahisi faraja na kuona kuwa ipo siku atafanikiwa katika maisha.
"Kazi hii naitamini kama ajira nyingine kwani inanifanya nipate mahitaji yangu ya kila siku ikiwa pamoja na kuwasomesha watoto wangu ili wapate elimu ambayo itakuja kuwa mkombozi wao katika maisha yao ya baadae",alisema Mama Hassani.
Alisema moja ya changamoto inayowakabili ni pamoja na bei za dawa kwa ajili ya kuua wadudu katika shamba lao kuwa juu huku akiiomba Serikali kuwapunguzia bei ya pembeo hizo zikiwemo mbegu.
No comments:
Post a Comment