Mbinu za kufanikiwa barani Afrika
Elimu ni ufunguo wa maendeleo ya Afrika lakini katika maeneo kadhaa shule na vyuo vikuu bado ni vichache. "Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako" kinaleta elimu katika kila eneo la bara hilo.
Maisha yanabadilika kwa haraka katika bara la Afrika: Mtandao wa Internet pamoja na matumizi ya simu za mkononi yanazidi kukua, lakini maelfu ya watu bado wametengwa na dunia ya vyombo vya mawasiliano. Vijana wa Kiafrika wanatafuta nafasi yao katika jamii ya dunia ambayo imejikita katika elimu na wanawaza ni njia gani itawafikisha katika kazi bora ama elimu bora. Kwa mfano, wengi wanajiuliza ni nafasi gani za elimu na mafunzo zinapatikana katika mtandao na ni nafasi gani utandawazi unaweza kusaidia. Maelfu kwa maelfu wanataka kwenda kupata elimu katika bara la Ulaya, lakini hawafahamu kile kitakachotokea huko waendako.
Taarifa na burudani
Deutsche Welle inataka kuleta tofauti. Kipindi cha "Deutsche Welle Learning by Ear - Noa bongo! Jenga maisha yako" kinaangalia changamoto ambazo anakabiliana nazo kijana wa Kiafrika na kinawaweka karibu wasikilizaji katika njia ya kupata taarifa pamoja na burudani. Vipindi hivi ni mchanganyiko wa ripoti zenye kina, michezo ya radio pamoja na taarifa za makala ambazo zitampa msikilizaji wake nafasi ya kupata mbinu muhimu za kuweza kufanikiwa katika Afrika ya leo na kugundua ulimwengu mpana wa elimu. Wasikilizaji walengwa ni wasichana na wavulana kuanzia miaka 12 hadi 20.
Uhusika
Vipindi vinatayarishwa na waandishi wa Kiafrika kutoka katika bara hilo, wakisaidiwa na wafanyakazi mahiri wa Deutsche Welle. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe. "Deutsche Welle Learning by Ear - Noa bongo! Jenga maisha yako" kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.
No comments:
Post a Comment