Na dijackson john
Mkoa wa manyara ni kati ya mikoa inayokabiliwa na uhaba wa
maji katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo, moja ya maeneo ambazo zina uhaba wa
maji ni pamoja na Kata ya Haydom iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Mbulu
na linalopatikana katika jimbo la uchaguzi la Mbulu vijijini.
Wakazi wa kata hiyo wapatao zaidi ya 10, 000 wanakuimbwa na
tatizo hilo kwa kipindi kirefu huku hata maji yanayopatikana kwa shida huwa ya
magadi (Maji ya chunvi) , huduma ya maji hupatikana karibu kilomita 7 hadi 10
kutoka makazi ya watu zilipo. Wakazi wa kijiji cha Gidarudagaw kinachpakana na
kijiji cha Endaharghadat hususani wale wanaoishi kaskazini mwa kijiji cha
Gidarudagaw hutafuta huduma ya maji kwa taabu kwani maji hayo hupatikana katika
mto uitwao Endabash karibu kilomita 10 , mto mwingine ni mto Mewadan unaotokea
katika mto uitwao Qorong’ayda karibu kilometa 7 kutoka kwa wakazi hao na maji
yake ni Chunvi.
Katika maeneo ya mjini maji yanapatikana katika vioksi huku
adha kubwa ikiwa kukatika mara kwa mara kitendo kinacho sababisha kuwa na
foleni kubwa ya watu inayoanza kujitokeza kuanzia mida ya saa kumi usiku.
Mwananchi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema “ni lazima niwahi
alfajiri kuwahi nafasi kwa sababu nikichelewa ni vigumu kupata maji mapema , chakushangaza
utakaa hadi saa saba mchana bado ujateka maji , au unaweza kufika hapa kuchota
maji asubuhi mhudumu akija akifungua bomba basi maji hayatoki , hii inatuathiri
sana hasa katika shuguli za uzalishaji”
Katika kampeni za uchaguzi mkuu iliyomalizika hapo octoba 25
mwaka jana kwa wananchi kuwachagua viongozi moja ya ahadi zilizopewa uzito na
wagombea ilikuwa juu ya suala la upatikanaji wa maji katika kata hiyo na maeneo
ya jirani , diwani wa kata ya Haydom Bw. Elibariki Marceli alisema “Suala maji
katika kata yangu ni tatizo kubwa nitahakikisha tuwapo barazani suala hili
nalishughulikia kikamilifu.”
Kipindi cha mwaka 2010/2015 jitihada zilifanyika za
kupatikana maji katika eneo hilo la mkoa wa manyara , na hii ni mujibu wa
mbunge wa Mbuli vijijini Mh. Flatei Georgery ambaye alifafanua hili kwa undani.
No comments:
Post a Comment