Tuesday, March 1, 2016

Burundi: serikali yakubali kuwepo kwa makaburi ya halaiki

Mwili usiojulikana wa mtu aliouawa katika moja ya wilaya za mji wa Bujumbura nchini Burundi, Desemba 12, mwaka 2015.
Mwili usiojulikana wa mtu aliouawa katika moja ya wilaya za mji wa Bujumbura nchini Burundi, Desemba 12, mwaka 2015.
REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Na RFI
Baada ya ugunduzi wa kaburi la halaiki katika kata ya Mutakura wilayani Cibitoke kaskazini mwa mji mkuu Bujumbura, Meya wa mji wa Bujumbura amewaambia waandishi wa habari kuwa utawala ulizika miili 58 baada ya mashambulizi dhidi ya kambi za kijeshi Desemba 11 mwaka 2015.

Kwa mujibu Freddy Mbonimpa, miili 8 ya watu waliouawa ilizikwa katika makaburi yanayojulikana ya Kanyosha (kusini mwa mji mkuu Bujumbura) na 50 katika makaburi ya Mpanda (wilayani Gihanga katika mkoa wa Bubanza - magharibi mwa Burundi). Meya wa mji wa Bujumbura ametoa wito kwa familia ziliopoteza ndugu zao kumuona ili wape maelezo zaidi.
AU yafutilia mbali tangazo la Rais Jacob Zuma kwa niaba ya Ujumbe wake
Ujumbe wa viongozi wa Afrika ambao ulitembelea hivi karibuni nchini Burundi umetoa wito kwa ajili ya "mazungumzo bila masharti" ili kuindoa nchi hiyo katika mgogoro unaoikabili.
Viongozi wa Afrika "wamezialika pande zote katika mgogoro wa Burundi kushiriki katika mazungumzo hayo, bila masharti na kwa kuheshimu mkataba wa amani wa Arusha"uliokomesha vita vya wenyewe viliodumu zaidi ya mwongo mmoja (1993-2006), kwa mujibu wa tangazo hili mpya.
Viongozi hao wa Afrika "wamempongeza" mpatanishi kutoka Uganda, Rais Yoweri Museveni, na kumtaka "atangaze mwanzoni mwa mwezi Machi tarehe ya kuanza haraka kwa mazungumzo baina ya Burundi."
Umoja wa Afrika (AU) ulituma ujumbe wake nchini Burundi wiki iliyopita. Ujumbe huo uliongozwa na Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na uliundwa na marais wa Mauritania, Senegal, Gabon na waziri mkuu wa Ethiopia, ulilifanya ziara mjini Bujumbura Alhamisi na Ijumaa kujaribu kutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa unaoikumba Burundi kwa kipindi cha miezi 10 sasa.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kushoto) na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma (kulia) wakati wa hotuba ya kuhitimisha ziara ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika, tarehe 27 Februari.
AFP
Jumamosi wiki iliyopita, kwa niaba ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais Jacob Zuma alitoa wito kwa kufanyika"mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote muhimu" katika mgogoro huo. Kauli ambayo ilielezwa kuwa haina maana yoyote, kauli ambayo haitatui suala muhimu la akina nani ambao wanatakiwa kushiriki katika mazungumzo hayo.
Bujumbura inaendelea kukataa mazungumzo yoyote na muungano wa wanasiasa waliokimbilia nje ya nchi (CNARED), ambao inautuhumu kuhusika katika vurugu zinazoendelea kushuhudiwa nchini Burundi.
Viongozi wote waliokua wakiunda Ujumbe huo wa Aumoja wa afrika, waliondoka tangu Alhamisi usiku na Ijumaa, ispokua Jacob Zuma, ambaye alibaki mjini Bujumbura kwa siku nyingine moja. Alikutana kwa mara nyingine tena na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Kabla ya kuondoka Jumamosi saa sita mchana, Bw Zuma alizungumza kwa niaba ya ujumbe mzima wa Umoja wa Afrika, jambo ambalo "limeushangaza" Umoja huo, chanzo cha kidiplomasia kutoka Umoja wa Afrika,ambacho hakikuta jina lake litajwe, kimeliambia shirika la habri la Ufaransa.

No comments:

Post a Comment