Tuesday, March 1, 2016

Afrika Kusini: Bunge lakataa kufuta imani dhidi ya Rais Zuma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Februari 19 mwaka 2015, Bungeni, wakati akilihutubia taifa.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Februari 19 mwaka 2015, Bungeni, wakati akilihutubia taifa.
REUTERS/Mike Hutchings

Na RFI
Bunge la Afrika Kusini limefutilia mbali Jumanne hii hoja ya kutokuwa na imani dhidi ya rais wa Afrika Kusini lililowasilishwa na chama kikuu cha upinzani kwa lengo la kumtimua madarakani Rais Jacob Zuma.

Jacob Zuma anatuhumiwa kuitumbukiza nchi hiyo katika mdororo wa kiuchumi. Pendekezo la chama cha Democratic Alliance (DA), ambacho kinamtuhumu Rais Zuma kuwa alisababisha"uharibifu mkubwa wa uchumi," limepata kura 99 dhidi ya kura 225 ziliyopinga. Wabunge ishirini na mbili hawakupiga kura, Bunge linaundwa na idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha African National Congress (ANC), ambacho kiko madarakani tangu mwaka 1994.
Wabunge nchini Afrika kusini wamekutana Jumanne hii kujadili hoja ya kutokuwa na imani na rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, kabla ya kuipigia kura wakati huu upinzani nchini humo ukiendelea kumshinikiza bwana Zuma kujiuzulu, kufuatia tuhuma za ufisadi zinazomkabili.
Zuma anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa Euro milioni 15 fedha za umma kwa ajili ya kuifanyia ukarabati nyumba yake binafsi iliyopo katika eneo la Nkandla mashariki mwa nchi hiyo.
Vyama vya upinzani nchini Afrika Kusini ndivyo vilivyomfungulia kesi Zuma kutokana na hatua yake ya kutumia vibaya fedha za umma.
Hivi karibuni Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini ilithibitisha kutumiwa kiasi cha Euro milioni 15 kwa ajili ya kukarabari nyumba binasfi ya Rais Jacob Zuma kukiwemo kuimarisha hali ya usalama wa nyumba hiyo, kujenga bwawa la kuogolea, ukumbi wa michezo ya kuigiza na kadhalika.
Zuma amekataa kurejesha fedha hizo na kujifanya kutokuwa na taarifa kuhusu kitita hicho 

No comments:

Post a Comment