Saturday, March 5, 2016

Rwanda kujitoa katika mahakama ya Afrika

Hatua hiyo imekuja baada ya mawakili wa raia wa Rwanda Victoire Ingabire kuwasilisha ombi mbele ya mahakama hiyo la kuwapa fursa ya kuonana na mteja wao Ingabire anayetumikia kifungo katika moja ya magereza nchini Rwanda.
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rwanda imewasilisha barua katika mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iliyoko Tanzania ya kutana kukatisha ushirikiano na mahakama hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya mawakili wa raia wa Rwanda Victoire Ingabire kuwasilisha ombi mbele ya mahakama hiyo la kuwapa fursa ya kuonana na mteja wao Ingabire anayetumikia kifungo katika moja ya magereza nchini Rwanda.
Wakili wa mlalamikaji Shabai Ragate amesema amesikitishwa na hatua ya serikali ya Rwanda kushindwa kuwakilisha utetezi juu ya maombi ya mteja wao na badala yake wameleta barua ya kutaka kuondoa tamko la kuwaruhusu wananchi na taasisi za kiraia kupeleka mashauri yao kwenye mahakama hiyo.
Rais wa mahakama hiyo jaji Agustino Ramadhani amesema mahakama imepokea barua kutoka serikali ya Rwanda inayoeleza kuwa hatua yake ya kuondoa tamko hilo ikiwa tayarimahakama imeshapanga siku ya kusikiliza shauri hilo na kwamba hizo ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili mahakama hiyo na jambo kubwa ni kuona nchi zilizoridhia zinakuwa kikwazo.
Kifungu namba 34.6 kinasema kwamba kila nchi iliyoridhia kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni lazima itoe tamko la kuwaruhusu wananchi na asasi za kiraia kupeleka masuala yao katika mahakama hiyo.

No comments:

Post a Comment