MAHAKAMA YA AFRIKA YA
HAKI ZA BINADAMU YAFIKISHA MWAKA TANGU KUANZA KWAKE.
Na Jenesta Zedekia.
Mahakama ya Afrika ya
haki za binadamu mkoani Arusha imeazimisha kilele cha maadhimisho ya wiki
ya wanawake duniani mapema wiki iliyopita kwa kuwataka wanawake kuweza
kufika katika vyombo vya sheria ili kuweza kutambua haki zao za msingi katika
jamii.
Awali akifungua semina
hiyo ambayo imewajumuisha wananchi mbalimbali wakiwemo wanawake katika mahakama
ya Afrika ya haki za binadamu mkoani hapa Raisi wa mahakama hiyo Jaji Agustino
Ramadhani alisema mahakama itahakikisha wanawake wanafurahia haki zao za msingi
kwa kuhakikisha wanafuata itifaki za mahakama.
Nao baadhi ya wanawake
ambao pia wanajishughulisha na masuala ya kisheria akiwemo mkurugenzi wa jumuiya
ya wanasheria Zanzibar Jamila Muhamudu pamoja na Edda Barnabas ambaye ni
mkurugenzi wa shirika la Tanzania women children wolfie centre walisema kuwa
wanawake waweze kuwa na muamko wa kujua haki zao za msingi hususani kwa wale
wanaoishi maeneo ya vijijini huku wakidai
wanahitaji kuwa hamsini kwa hamsini katika jamii zinazo wazunguka.
“kutokana na kauli
mbiu ya mwaka huu inavyosema wanawake tuweze kuwa hamsini kwa hamsini katika
jamii basi tuweze kuwa mstari wa mbele katika kuinua pato la nchi kiuchumi na
kiutamaduni ili kuwa mfano bora kwani wanawake ni jeshi kubwa katika
jamii”.Alisema Jamila Muhamudu.
Nao wadau
mbalimbali wa sheria jijini Arusha walioudhuria katika semina hiyo akiwemo
mwanasheria wa kujitegemea ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wanasheria
kanda ya Arusha Modest Akida walieleza
umuhimu wa mwanamke kujua haki zake na kuzifuatilia ili kuweza kuzienenda
katika jamii.
“kwanza niseme
wanawake ni jopo kubwa katika jamii zetu isipokuwa hawajiamini wanapopatwa na
matatizo wanaogopa kufika katika vyombo vya sheria ndipo wanajikuta wananyimwa
haki zao katika jamii hususani katika ndoa zao”Alisema Akida.
Kilele cha maadhimisho
ya wiki ya wanawake duniani ufanyika kila ifikapo March,8 kila mwaka ambapo
wiki iliyopita maadhimisho hayo yalifanyika
katika mahakama ya Afrika ya haki za binadamu mkoani Arusha ambapo pia ni miaka
kumi tangu kuanza kwa mahakama hiyo.
No comments:
Post a Comment